Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Diamond amemsusa Lavalava WCB?? kwanini yupo kimya sana??

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameennda na Lava lava kutoka WCB Wasafi baada ya ukimya wake kwa ndani ya miezi 10 bila kutoa ngoma yake kama ilivyokuwa zamani.

Sio tu kukaa kimya bali amefuta post zote kwenye page yake ya Instagram bila kueleza sababu maana wasanii wengi hueleza kama wanatoa album au kitu fulani ila yeye hajatoa taarifa yoyote.

Lava lava umepita muda sasa haonekani na wasanii wenzake kutoka katika lebo yake na hata majuzi tumeona wasanii wa WCB wakiongozwa na Diamond kwenda kufanya show Mbagala lakini yeye hakuwepo.

Ngoma ya mwisho ya Lavalava ni DESH DESH ambayo ilitolewa miezi 10 iliyopita, kitu ambacho sio cha kawaida kwa wasanii wa WCB kukaa kimya kwa muda hivi bila ngoma.

Angalia upande wa Zuchu pia angalia upande wa Mbosso na hata boss wao Diamond wannavyoachia kazi lakini kwa Lava lava imekuwa tofauti sana.

Unahisi ukimya wa Lava lava unasababishwa na nini?? amesuswa na lebo yake ya WCB?? anafanya kazi zake binafsi nje ya lebo yake??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents