Burudani

Diamond kutua Mwanza na FOA tour wikiendi hii

Staa wa muziki wa Bongo Fleva @diamondplatnumz anatarajiwa kuendelea na Tour yake kwa ajili ya kuitangaza EP yake ya #Foa ambapo wikiendi hii atapiga Show Mwanza.

Ikiwa ni kituo chake cha tatu kati ya vituo 17 alivyovitangaza kuwa atazunguka kwa ajili ya Tour ya Ep yake baada ya kupiga show Ephiopia, Abidjan nchini Ivory Coast na sasa ni Mwanza Tanzania.

Mwanza ndio sehemu pekee Tanzania ambayo @diamondplatnumz ameamua kufanya show kwa ajili ya EP yake ambayo itafanyika @the_cask_bar_grill

Katika orodha ya sehemu ambazo @diamondplatnumz alizotangaza kwa ajili ya Show ambazo bado ni Lagos Nigeria, Istambul Uturuki, Laussane Uswisi, Ureno, Brussels Ubelgiji, Helanki Finland, Copenhagen Denmark, Oberhausen Ujerumani, Stockhom Sweden, Toronto Canada,London Uingereza na Freetown Sierra Leone.

Unahisi Mwanza inatosha kwa ajili ya Tour ya FOA Tanzania au aongeze mkoa mwingine ?

Dondosha Comment yako hapa chini. #Bongo5Updates

Related Articles

Back to top button