Diamond na Zuchu Mke na mume?? Amuita mke wangu
Tarehe 23 mwezi huu wa 11 tunajua ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Zuhura Othman Soud alimaarufu Zuchu, katika siku hii ya kuzaliwa ya inawezekana ndio ikawa siku kubwa zaidi kwenye maisha yake kwani boss wake Diamond Platnumz siku ya jana alimtakia heri ya siku ya kuzaliwa na kuonyesha ulimwengu namna anavyompenda Zuchu.
Katika vitu ambavyo wengi walikuwa na wasiwasi kuwa Diamond na Zuchu wapo kwenye mahusiano au laah naamini siku ya jana walipata uhakika wa asilimia 90 kuwa wapo kwenye mahusiano baada ya Diamond kupost video wakiwa Gym na wakiwa kwenye mazingira ya kuonyesha wapo kwenye dimbwi la mapenzi
Mbali na hilo usiku wa kuamkia leo Jux alikuwa anafanya Listening Party ya Album yake ya King of Heart, ngoma ya Jux aliyomshirikisha Zuchu inaitwa NIDHIBITI alienda mbele Diamond kuitambulisha na katika utambulisho huo alisema hii ndio ngoma yangu pendwa kwani Juma amemshirikisha Mke wangu ambaye mke mwenyewe ni Zuchu.
Kuanzia leo tayari wengi wameamini kuwa Diamond na Zuchu wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi baada ya kauli hiyo.