Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzFahamuHabari

Diamond Platnumz mfalme wa Youtube kusini mwa jangwa la Sahara

Wanamuziki 10 bora wa Afrika wanaoongoza zaidi katika mtandao wa Youtube kwa kuwa na wafuasi wengi kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan) Diamond kinara.

Jina la Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania ndio kinara katika orodha ya wasanii hao ambao wanatoka ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara.

Diamond ameshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Subscribers zaidi ya Milioni 6.84 kwenye chaneli yake tangu ilipoanzishwa mwaka 2011.

Kwa ufupi wasanii watatu wa juu wote wanatokea Tanzania ambao ni Diamond Platnumz, Rayvanny na Harmonize.

 

Mfalme wa Bongo Fleva na Boss wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz pia amepata maoni zaidi ya Bilioni 1.6 kwenye Chaneli yake.

Namba mbili kwenye orodha hiyo niĀ  Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Next Level Music, Raymond Shaban Mwakyusa, anayefahamika zaidi kwa jina la Rayvanny ambaye ana wateja zaidi ya Milioni 3.91. akipata maoni zaidi ya milioni 677.

Namba tatu ni Harmonize akiwa na wafuasi milioni 3.39 halafu namba nne ni Ckay kutoka nchini Nigeria akiwa na wafuasi milioni 3.07.

Kwa orodha hii unahisi kwanini wasanii wa Tanzania wanakuwa wakubwa Youtube na sio kwenye platform zote za muziki Afrika??

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents