Habari

Diamond, Rayvanny na Nandy washinda tuzo kubwa nchini Marekani

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz usiku wa kuamkia leo Jumapili ameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) kwenye kipengele cha ‘Best Collaboration Award’ kupitia wimbo wake wa Baila.

Kwenye kipengele hicho Diamond ameshinda na mwenzie @miribenari ambaye ndiye aliyemshirikisha kwenye wimbo huo, Hata hivyo Diamond hakuwepo kwenye sherehe hizo na tuzo yake ilipokelewa na Miri Ben-Ari.

Wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni Rayvanny na Nandy kwenye vipengele vya Best Male/Female in East, South and North Africa.

Pia Mtangazaji wa kituo cha Times FM, Lil Ommy naye ameshinda tuzo ya ‘Best Host’, Huku Babu Tale akichukua tuzo ya Meneja bora wa wasanii barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents