Habari
Dk. Biteko awasili nchini Kenya kwa ziara ya kikazi
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika ( US-Africa Nuclear Energy Summit).
Mkutano huo wa masuala ya Nyuklia utahusisha mijadala kuhusu utayari wa Sekta ya Nishati katika kusimamia mnyororo wa thamani kwa ajili ya uendelezaji wa nyuklia pamoja na umuhimu wa kuwashirikisha wanawake na vijana katika Sekta.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameambatana na Watendaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.
Written by Janeth Jovin