Habari

Dkt. Mpango akemea unyanyasaji, ukatili maeneo ya kazi

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekemea vitendo vya uonevu, unyanyasaji na ukatili katika maeneo ya kazi, ambavyo husababisha wafanyakazi kudhalilishwa na kuwa wanyonge.

Dkt. Mpango ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za mwajiri bora wa mwaka 2022, zinazoratibiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Amesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na vinaathiri utendaji wa kazi sio tu kwa waathirika, bali kwa viongozi na taasisi au mashirika wanayofanyia kazi.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kila mfanyakazi ana haki ya kutendewa utu, kuthaminiwa na kuheshimika kazini.

Ameagiza kuwekwa mifumo itakayowezesha wafanyakazi kutoa taarifa za kunyanyaswa au kuonewa bila kuhofia madhara yoyote yanayoweza kujitokeza ikiwemo kupoteza ajira zao.

Kwa upande wa waajiri nchini, Dkt. Mpango amewasihi kuzingatia sheria na kutoa mikataba ya kazi kwa kazi zinazostahili mikataba badala ya kuwafanyisha watu kazi kama vibarua kwa kazi ambazo wangeweza kupata mikataba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents