HabariSiasa

Dola bilioni 1.39 zachangishwa kukabiliana na ukame Ethiopia, Kenya na Somalia

Mkutano wa wahisani uliofanyika mjini Geneva umechangisha dola bilioni 1.39 kwa ajili ya eneo la Upembe wa Afrika, ambalo hali inayoendelea ya ukame inatishia mamilioni ya watu na ukosefu mkubwa wa chakula.

Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kiutu – OCHA imesema fedha zilizochangishwa zitatumika katika miradi ya kiutu na maendeleo nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, huku eneo hilo likikumbwa na hali mbaya zaidi ya ukame kuwahi kutokea katika miaka 40.

Mashirika ya kibinaadamu yalikuwa yameomba dola bilioni 1.4 kwa ajili ya miradi mbalimbali katika eneo hilo.

Umoja wa Mataifa umesema fedha zilizoahidiwa jana zitatumiwa na mashirika ya kiutu kutoa chakula cha dharura, msaada wa kiafya pamoja na chakula cha mifugo na dawa za kuwaweka hai wanyama hao.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu milioni 6 nchini Somalia wanahitaji kwa dharura chakula, pamoja na milioni 3.5 nchini Kenya na milioni 6.5 nchini Ethiopia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents