Uncategorized

Dola bilioni moja za changwa kwaajili ya Notre Dame, Rais wa Ufaransa atangaza miaka 5 ya ujenzi wa kanisa hilo la karne ya 12

Kiasi cha fedha dola bilioni moja kimechangishwa kutoka kwa waumini wa kawaida na watu wenye uwezo na umaarufu kutoka duniani kote kwa ajili ya ujenzi mpya wa kanisa kuu la kihistoria la Notre Dame mjini Paris nchini Ufaransa baada ya kuharibiwa vibaya na moto.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameongeza shinikizo kwa kutangaza muda wa miaka 5 wa kukarabatiwa upya kanisa hilo la karne ya 12.

Leo Rais Macron anaendesha kikao maalum cha baraza la mawaziri kitakachojikita katika suala la tukio la moto la Notre Dame.

Image result for Notre Dame


Mjumbe anayehusika na turathi na utamaduni Stephane Bern ameliambia shirika la habari la kifaransa la France Info leo kwamba dola milioni 995 zimeshachangishwa mpaka sasa ambapo wachangiaji ni watu maarufu wakiwemo wamiliki wa makampuni makubwa ya urembo ya L’Oreal, Chanel na Dior. Maafisa wanalichukulia tukio hilo la moto kama ajali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents