Dola zaidi ya laki mbili zadaiwa ili kulala jela kama Mandela

Taasisi isiyo ya kiserikali nchini Afrika Kusini, imetoa ofa ya watu kulala katika jela alilofungwa Baba wa taifa hilo, Nelson Mandela, alipotumikia kifungo cha miaka 27.

Tafrija inayoandaliwa na ‘ CEO Sleepout’, inapokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali hadi itakapofika uiku wa Julai 17, ambapo watatangaza washindi wa zoezi hili la kulala jela.

Ofa zinazopokelewa ili kuwawezesha wadau mbalimbali kulala jela ya Mandela, zinaanzia kiwango cha chini cha dola 250,000, sawa na zaidi ya milioni 550 za Kitanzania.

Hii ni mara ya kwanza tangu tukio la sampuli hii kufanyika Afrika Kusini, katika kuienzi siku ya kuzaliwa ya marehemu Nelson Mandela, ya Julai 18.

Kati ya fedha zitakazopatikana kutokana na zoezi hili, zitakwenda kuwasaidia wafungwa kupata elimu ya kiwango cha chuo kikuu.

Mpaka sasa, wameshapatikana watu watatu waliojisajili kushiriki zoezi hili la kulala jela.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button