Dozi 115,200 za chanjo ya Janssen zawasili nchini

Tanzania imepokea shehena ya Chanjo ya Janssen Dozi 115,200 kutoka Serikali ya Ubeligiji kupitia mpango wa COVAX utaosaidia kuchanja wananchi 115,200 dhidi ya UVIKO-19.

Akipokea chanjo hizo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema chanjo hiyo ni ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji kupitia mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa kupambana na maambukizi ya UVIKO – 19 (Covax Facility).

Hii ni awamu ya tatu kwa chanjo aina ya JANSSEN kupokelewa nchini kupitia mpango wa COVAX.

Aidha Waziri Gwajima amesema chanjo dhidi ya UVIKO – 19 zipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali, na kutoa rai kwa wale ambao bado hawajapata chanjo kwenda kupata chanjo hiyo.

Related Articles

Back to top button