HabariSiasa

DR Congo wamuomboleza Lumumba

Nchini DRC, mambolezo ya kitaifa yanaendelea baada ya kuwasili kwa mabaki ya mpiganiaji wa  uhuru  Patrice Lumumba ambaye jino lake lilirejeshwa na nchi ya Ubelgiji, Juni tarehe 20. Ubelgiji alikuwa mkoloni wa nchi hiyo.

Mabaki ya Lumumba  aliyeuawa miaka 61 iliyopita, yamekuwa yakizungushswa nchini humo na yamewasili jijini Kinshasa baada ya kutokea Lubumbashi.

Maelfu walijitokeza huku milio ya ngome za kitamaduni zikisikika na ibada kufanyika kumwombea Marehemu Lumumba.

Profesa Célestin, ni rafiki ya Lumumba, mzaliwa wa Sankuru alikozaliwa mpambaniaji huyo wa uhuru.

“Kweli tumeguswa sana kuona mabaki yake yanapita pale alipouliwa.  Alizaliwa mahali pengine na leo mazishi yake umefanyika hapa.  Kwetu sisi, huu ni wakati wa ishara, wenye umuhimu mkubwa,” alisema.

Nao wananchi wa DRC waliohudhuria wamekuwa na kumbukumbu nyingi.

“Tunamkumbuka sana  Lumumba, alifanya mengi kwa ajili ya nchi yetu, “ Mmoja amesema, mwananchi mwingine naye ameeleza kuwa, “Siwezi kumsahau mpambanaji huyu kimekuja hapa kutoa heshima za mwisho,” ameeleza akiangua kilio.

Mbali na heshima za mwisho, Lumumba, amejengewa mnara wenye thamani wa Dola Milioni mbili na Laki Nne, jijini Kinshasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents