HabariMichezo

Drogba- Ahmed Ally ambatiza jina Kibu Denis

Tangu Kibu Denis kuifunga #YangaSC goli kwenye mchezo wa Derby ya Kariakoo na kushangilia kwa aina yake nyota huyo amekuwa akifananishwa na Staa wa Chelsea Didier Drogba.

Wapenzi wa soka hususan wa #SimbaSC wamekuwa wakimfananisha kutokana na Umbile lake, mtindo wa kushangilia, wingi wa nywele kichwani na wakati mwingine hukumbushia ‘shuti alilopiga’ lililo mshinda kipa wa Yanga Djigui Diarra.

Katika kunogesha hilo Meneja Habari wa Simba Ahmed Ally amemvika rasmi jina la Drogba.

Kupitia ukurasa wake Ahmed ameandika “Kibu Drogba ametembelea Uwanja wa Nangwanda ameridhishwa na nyasi zake amesema zinamruhusu kupiga mashuti na ku slide bila kuuumia.”

Je jina la Drogba linamfaa Kibu Denis.?
Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents