Fahamu

Dubai yatengeneza mvua feki kukabiliana na joto (+ Video)

Dubai inapitia kipindi kigumu cha hali mbaya joto kali. Eneo hilo ndani ya Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) lina joto joto linavuka mpaka nyuzijoto 50 na kuhatarisha maisha ya watu zaidi ya milioni 3 wanaoishi katika mji huo.

Hivi karibuni nchini Canada zaidi ya watu 500 waliripotiwa kufariki dunia kwa sababu ya joto kali. Kuepuka madhara hayo UAE) kupitia kitengo cha hali ya hewa kimekuja na teknolojia inayoweza kupunguza hali hiyo ya joto, na teknolojia hiyo ni utengenezaji wa mvua feki.

 

Kituo cha hali ya hewa cha nchi hiyo kupitia tovuti yake, wiki hii kilichapisha video kupitia mtandao wake wa twitter ikionyesha mvua hiyo kubwa kiasi iliyokuwa inanyesha kwenye maeneo kadhaa huku watu wakiendelea na maisha yao ya kawaida na magari yakionekana yakipita kwenye barabara kubwa zenye mvua.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CRqsCaajIqL/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents