BurudaniHabariMahojiano

Dudu baya alilogwa?? alikuwa hawezi kwenda haja kubwa na ndogo

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Dudu Baya amezungumza kwa mara ya kwanza na @el_mando_tz kuhusu maradhi ya ajabu yaliyomkumba. Dudu Baya kwenye mahojiano hayo na @el_mando_tz amezungumza kwa urefu sana na kusema maradhi yalianza tangu 2021.

Dudu bya amesema kuwa Miguu yake ilikosa nguvu na mwili mzima alikuwa hawezi kusimama hata haja kubwa na ndogo alikuwa hawezi kwenda.Dudu baya anasema hawezi kuacha Harakati za kupigania maslahi ya wasanii wasio na nguvu ambao wananyonywa na wenye nguvu.

Akipiga story na @el_mando_tz amesema kuwa wasanii wengi sana wa Bongo Fleva wanaishi maisha kwenye vifungo vya maisha na ndio maana wengi wao wameingia kwenye maisha ya kutumia madawa ya kulevya kwa sababu ya mawazo.

Ameongeza kuwa msanii pekee Tanzania anayeishi maisha ya amani na ya furaha ni @officialalikiba

Ameongeza kuwa wasanii wengi wananyanyasika sana msiwaone wanapost magari ya gharama na majumba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents