Habari

ECOWAS yaondoa vikwazo kwa wanachama wake Mali, Guinea na Burkina Faso

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wameamua kusitisha adhabu dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Mali, Guinea na Burkina Faso.

Viongozi hao wamefikia uamuzi huo kwenye mkutano wa kilele wa nchi za kanda ya Afrika Magharibi uliofanyika siku ya Jumamosi.

Viongozi hao walikutana kwenye mji mkuu wa Ghana, Accra kufanya maamuzi iwapo wataongeza vikwazo au wataziondolea vikwazo nchi ambazo zilikabiliwa na vikwazo na hatua nyingine za kinidhamu katika kanda hiyo.

Rais wa Tume ya ECOWAS Jean-Claude Kassim Brou amesema mataifa15 wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS yamepanga kukutana tena tarehe 3 mwezi ujao wa Julai kubaini ikiwa nchi hizo tatu zilizosimamishwa uanachama wao za  Mali, Guinea na Burkina Faso zitawekewa vikwazo vingine.

ECOWAS tayari imeweka vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ya Mali mnamo mwezi wa Januari ambavyo vimetatiza biashara nyingi, pamoja na kufungwa kwa mipaka ardhini na angani kati ya Mali na nchi nyingine katika eneo hilo la Afrika Magharibi.

Hatua hizo zimeudhoofisha mno uchumi wa Mali, na kusababisha wasiwasi juu ya kuzuka kwa mgogoro wa kibinadamu utakaoleta na madhara kwa raia wa Mali. Licha ya vikwazo hivyo dhidi ya Mali hakuna mafanikio yoyote ya kisiasa yaliyopatikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents