BurudaniFahamuHabari

Ed Sheeran angetakiwa kumlipa Marvin Gaye zaidi ya Tsh bilioni 230 kwa Copyright

Siku ya jana Mahakama ya Manhattan, New York nchini Marekani ilitoa uamuzi wa kesi iliyokuwa ikimkabili Staa wa muziki wa nchini Uingereza Ed Sheeran na kusema wimbo wake  “Thinking Out Loud” haukukiuka hakimiliki za wimbo wa Mwimbaji wa Marekani Marvin Gaye “Let’s Get It On.”

Mahakama ilisema Ed Sheeran alitunga na kutengeneza wimbo wake kwa kujitegemea na hakuna kipengele chochote kwenye utunzi wa nyimbo hiyo kilichotoka kwenye wimbo wa Marvin Gaye.

Kesi hii ilishika kwenye headlines duniani baada ya mashtaka hayo dhidi ya Ed Sheeran kufunguliwa mwaka 2017 ila hatimaye uamuzi ulitolewa mapema hii leo kuhusu sakata hili ambalo Ed Sheeran aliwahi kuweka ahadi ya kuacha kufanya muziki endapo angekutwa na hatia ya kuiba wimbo wa Marvin Gaye.

Ndugu wa mtunzi mwenza wa nyimbo ya Marvin Gaye walimfungulia kesi Sheeran wakidai kwamba mdundo wa sauti wa nyimbo hizo mbili ulikuwa unafanana wakisema Ed Sheeran alikiuka hakimiliki ya wimbo yao ambapo kama Ed Sheeran angekutwa na hatia angetakiwa kuwalipa Walalamikaji dola milioni 100 kama fidia ambazo ni zaidi ya bilioni 233 za Kitanzania

Baada ya kusikiliza nnyimbo zote mbili unahisi kulikuwa na Copyright au jamaa Ed Sheeran kuna vitu aliiga??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents