Habari

Elon Musk alitoa $2bn ya hisa za Tesla kutengeneza magari ya umeme

Afisa mkuu mtendaji wa Tesla Elon Musk anasema alitoa hisa zenye thamani ya $1.95bn (£1.6bn) za kampuni yake ya kutengeneza magari ya umeme kwa shirika la hisani mwaka jana.

Mchango huo wa hisa milioni 11.6 ulielezewa katika jalada na wadhibiti wa Marekani kama “zawadi halisi”.

Wasilisho hilo halikutaja mpokeaji, au wapokeaji, wa mchango.

Pia mnamo Jumatano, Bw Musk alisema kuwa kuelekea mwisho wa mwaka huu itakuwa “wakati mzuri” kupata mtu wa kumrithi kama afisa mkuu mtendaji wa Twitter.

Hati iliyowasilishwa kwa Tume ya Usalama na Ubadilishanaji wa Fedha ya Marekani ilionyesha mchango huo ulitolewa kati ya Agosti na Desemba mwaka jana.

Tesla haikujibu mara moja ombi la BBC la kutoa maoni.

Sio mara ya kwanza kwa Bw Musk kutoa hisa za Tesla kwa uhisani. Alichangia hisa zenye thamani ya $5.74bn mnamo 2021, kulingana na jalada la udhibiti .

Pia alisema kwenye Twitter mwaka huo , kwamba alipanga kuchangia $20m kwa shule katika Kaunti moja ya Cameron na $10m kwa jiji la Brownsville huko Texas kwa ajili ya “kufufua jiji”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents