Technology

Elon Musk: Sina uhakika kama ntafanikiwa kuinunua kampuni ya Twitter

Mkuu wa Tesla Elon Musk amesema “hana uhakika” kama zabuni yake ya kutwaa kampuni ya mitandao ya kijamii ya Twitter itafanikiwa.

Alitoa maoni hayo katika mkutano saa chache baada ya kufichua kwamba alijitolea kununua kampuni hiyo kwa $54.20 kwa hisa, au zaidi ya $40bn (£30.6bn).

Pia mnamo Alhamisi, Mkurugenzi mkuu wa Twitter aliwaambia wafanyakazi kwamba kampuni hiyo ilikuwa ikitathmini ombi la zabuni hiyo.

Parag Agrawal pia aliripotiwa kusema katika mkutano wa wafanyakazi kwamba kampuni “haijashikiliwa mateka” na ofa hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa TED2022 huko Vancouver, Bw Musk alisema: “Sina uhakika kwamba nitaweza kuipata.” Aliongeza kuwa alikuwa na Mpango mbadala ikiwa ombi lake la Twitter litakataliwa, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Bw Musk pia alisema katika hafla hiyo kwamba Twitter inapaswa kuwa wazi na wazi zaidi. “Nadhani ni muhimu sana kuwepo na uwanja jumuishi wa uhuru wa kujieleza,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents