Eng. Hersi aeleza gharama za Yanga kwenda Afrika Kusini

Rais wa Klabu ya Yanga Engineer Hersi Said ameeleza gharama ya safari ya timu hiyo kwenda Afrika Kusini kwenye mechi klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns itakayocheza leo Ijumaa.
Hersi akiongea na chama cha waandishi wa habari wa Afrika Kusini (SAFJA) amesema safari yao inagharimu Dola za Kimarekani 80,000 (Tsh Milioni 206).
“Ni gharama sana kuendesha klabu ya mpira wa miguu, ninaweza kukuambia safari yetu kuja Afrika Kusini kucheza na Mamelodi Sundowns inagharimu USD 80,000” alisema Eng Hersi.
“Tiketi ya kwenda na kurudi kwa mtu mmoja ni USD 600 na nimekuja na watu 50, hiyo ni USD 30,000 Watu 50 mara USD 150 kwa siku zidisha kwa siku nne, hiyo ni USD 30,000 nyingine.
“Hapo hujanunua kitu chochote na gharama za hoteli, unatakiwa kuzunguka hapa na pale baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kupewa posho wanaposafiri.
Imeandika na Mbanga B.