Michezo

Eng. Hersi anatafuta Kiki tu – Jemedari Saidi

Mchambuzi mkongwe wa soka la Bongo Jemedari Said ameweka wazi kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki alishasaini kuendelea kuwatumikia Wananchi kitambo na kilichokuwa kinaendelea mitandaoni ni kiki tu.

Kupita ukurasa wake wa Instagram Jemedari ameposti picha ya nyota huyo na kushusha maneno haya:

Tarehe 12 Juni Aziz Ki aliwekewa pesa za Kitanzania Tshs 520M kwenye benki moja hapa nchini na maelezo yake yalikuwa ni pesa ya usajili ambayo haikuanisha ni muda gani aidha mwaka au miaka miwili.

Pesa ambayo mhusika pia aliitoa badae kwa matumizi yake mwenyewe kwenye siku hiyohiyo.

Kinachoendelea mtandaoni ni jambo Jema Sana kwenye Dunia ya mitandao ili kuleta mvuto na kutengeneza wasiwasi kwa wanayanga na baadaye Viongozi kuibuka Mashujaa kwa kushinda Vita ya Usajili lazima kutengeneza kufuatiliwa kwenye Social Media platforms za klabu kwenye dunia ya leo.

Mchezaji ambaye hajasajiliwa amekuja kufanya nini kiasi apewe na muda kwenye App ya klabu? Welcome Back King Ki, the World is all yours. Hongera viongozi kwa kumbakisha Top Scorer.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents