HabariMichezo

Eng. Hersi: Coastal Union ni hatari nje ya Dar, tuombe Mungu

Kuelekea mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup kati ya Yanga SC dhidi ya Coastal Union, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said amewataka wanayanga kumuomba Mungu huku akisema kuwa Coastal Union ni tishio zaidi wakiwa nje ya Dar es Salaam.

“Coastal Union ni hatari zaidi kukutananao kwenye viwanja ambavyo sio vya Dar es Salaam” maneno ya Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said

Hersi ameongeza kuwa ”Mchezo utakuwa mzuri ila tumuombe Mungu tuweze kuchukua Ubingwa kwetu sisi ni muhimu zaidi,”

Fainali hiyo ya Azam Sports Federation Cup kati ya Yanga SC dhidi ya Coastal Union itapigwa kwenye dimbani la Sheikh Amri Abeid, Arusha Julai 2, 2022.

Imeandikwa na Hmaza Fumo, Instagram @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents