Michezo

EPL wakubali kutumia sheria mpya

Ligi Kuu ya England maarufu kama Premier League itaanza kutumia teknolojia ya kung’amua kama mchezaji yupo kwenye eneo la kuotea “Offside” inayojulikana kama Semi-Automated Offside technology.

Uamuzi huo umefanikiwa mchana wa leo baada ya klabu zinazoshiriki ligi hiyo pendwa duniani kukubaliana na mpango huo ambao unatazamiwa kupunguza utata zaidi katika masuala hayo ya offside.

Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Ligi hiyo inaeleza kuwa vilabu vimekubaliana kwa kauli moja kuanzishwa kwa teknolojia hiyo inayotazamwa kuleta urahisi wa kugundua matukio hayo kwa waamuzi na kuongeza ladha mpya na kuondoa utata hasa kwa wafuatiliaji wa ligi hiyo kwa njia ya Televisheni.

Teknolojia hiyo ilitumika kwa ufanisi mkubwa katika kombe la Dunia la FIFA 2022 lilofanyika nchini Qatar na inakuwa teknolojia ya tatu kubwa kuingizwa kwenye Soka baada ya teknolojia ya mstari wa goli, (Goal line Teknology) na teknolojia ya usaidizi wa waamuzi kwa video (Video Assistant Referee)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents