
Erik ten Hag ameionya Manchester United kuwa inaweza kurudi nyuma kama ilivyo kwa Chelsea kama pesa za timu hiyo hazitatumika vizuri kwenye usajili.
Ten Hag ameahidi kutumia pesa nyingi zaidi mara tu familia ya Glazer itaamua kuiuza timu hiyo kwa Sir Jim Ratcliffe au Bilionea wa Qatari, Sheikh Jassim bin Hamad Al-Thani.
Kuhusu Man United kutaka kumsajili Neymar, Kocha Ten Hag amesema kuwa ukifika muda sahihi atalizungumzia hilo.
Ingawaje Chelsea inapitia wakati mgumu tangu kuongozwa na Todd Boehly ambaye ameinunua kutoka kwa Roman Abramovich kwa pauni bilioni 4.25 imeshatumia karibu pauni milioni 600 kusajili wachezaji wapya.
Alipoulizwa kama Chelsea ni mfano wa jinsi timu zinapobadili uongozi wake unasababisha matatizo, Ten Hag alijibu: ‘Kweli, ndiyo, kama hakuna mikakati nyuma yake, pesa haifanyi kazi.”