HabariMichezo

Erling Haaland avunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy nakuweka yake PL

Erling Haaland amevunja rekodi nyingine kwenye Premier League wakati akiwaadabisha Wolves kwa kuwafunga hat-trick na Man City ikiondoka na ushindi mnono wa goli 3-0.

Haaland ameandika rekodi kwakufunga hat-trick nne akiwa amecheza michezo 19 pekee na kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Ruud van Nistelrooy ambaye yeye alifunga hat-trick hizo baada ya kucheza mechi 65.

Staa huyo wa Manchester City amekuwa kwenye kiwango kikubwa sana tangu kusajiliwa na Manchester City kipindi cha majira ya joto.

Mchezaji huyo kwa sasa anafukuzia kiatu cha dhahabu akiwa na jumla ya magoli 31, wakati msimu uliyopita aliyeshinda kiatu hicho alikuwa na mabao 24 tu.

Imeandikwa na @fumo255

 

Related Articles

Back to top button