Etoo ataka Tanzania iwe na timu nane Mashindano ya CAF
Samuel Etoo amesema Mataifa yenye Nguvu kisoka ngazi ya Vilabu kama Tanzania yanapaswa kuwa na timu 4 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Rais huyo wa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT) amesema hayo wakati akizungumza kupitia Mahojiano na kituo cha Televisheni cha RTI 1.
“Nafikiri ni wakati sahihi kubadili mfumo wetu wa upatikanaji wa vilabu katika Mashindano yetu ya CAFCL na CAFCC.
“Tunapaswa kufanya kama wanavyofanya watu wa Ulaya na Asia Mataifa yenye Ligi zenye nguvu hayapaswi kutoa timu sawa na Mataifa yenye Ligi dhaifu.”
“Mataifa kama Tanzania, Afrika Kusini, Congo DR, Senegal, Misri, Algeria, Morocco, Tunisia na Libya kwa sababu wanaligi bora wanapaswa kutoa Timu nne CAFCL na nyingine nne CAFCC.
“Endapo tutatumia mfumo huu utasaidia kuleta ushindani zaidi lakini pia kuongezeka kwa mashabiki wanaofuatilia Mashindano haya.
“Kila bara kwa sasa duniani linapambana kuongeza ushindani katika mashindano yao ya Vilabu na sisi Afrika tunatakiwa tubadilike kwa sababu binafsi naamini sisi waafrika ni Bora kisoka Duniani kuliko bara lolote lilr amesema Etoo”