FahamuVideos

EWURA watangaza kushuka kwa bei za mafuta mikoa hii mitatu (+ Video)

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushusha kwa bei za mafuta kwa mwezi January 2022 ukilinganisha na bei za mwezi Desemba 2021.

EWURA imesema Ikilinganishwa na bei za mwezi Desemba 2021, bei za Januari 2022 zitapungua kwa kati ya Shilingi 4 na 35 kwa lita ya petroli; na kati ya Shilingi 43 na 67 kwa lita ya dizeli isipokuwa kwa bandari ya Mtwara ambapo bei zitaongezeka kwa Shilingi 2 kwa lita; huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Shilingi 99 kwa lita.

Imesema Mwezi Oktoba 2021, Serikali ilipunguza tozo za taasisi za Serikali kwa lengo la kupunguza bei za mafuta hapa nchini.

Maamuzi hayo yamesaidia kupunguza bei za mafuta kwa kati ya Shilingi 23 na Shilingi 31 kwa lita kwa kutegemea aina ya mafuta na bandari yalipopokelewa mafuta hayo.

Vilevile, kutokana na kuendelea kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia, Serikali iliahirisha ukusanyaji wa ada ya mafuta (petroleum fee) kuanzia Desemba 2021 na hivyo kufanya bei ya juu kufikiwa katika mwaka 2021 kuwa ni Shilingi 2,510 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam, Shilingi 2,525 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Tanga na Shilingi 2,569 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.

Bila ya kufanya maamuzi haya, bei za mafuta zingefikia kiwango cha juu cha Shilingi 2,638 kwa lita ya petroli (Dar es Salaam), Shilingi 2,648 kwa lita ya petroli (Tanga); na Shilingi 2,693 kwa lita ya petroli (Mtwara).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents