Exclusive Interview: Bob Junior auzungumzia wimbo wake mpya ‘Kimbiji’ (audio)

Hivi karibuni niliandika maoni kuhusiana na video na wimbo mpya wa Bob Junior, Kimbiji yenye kichwa cha habari ‘Maoni: Kimbiji (Bob Junior): Video bora kwa wimbo wa kawaida?’

http://www.youtube.com/watch?v=oyJI9VMW8k4

Kwenye maoni hayo niliandika kuwa wimbo wa Kimbiji ni dance nusu na ungekuwa mkali zaidi kama ungetengenezwa kwa kuhusisha vyombo vingi kama zilivyo nyimbo za dance ama sebene.

“Hii si mara ya kwanza Man Walter kufanya wimbo wenye asili ya dance. Amewahi kutengeneza hit single ya Ali Kiba, Dushelele. Kwa haraka haraka Dushelele na Kimbiji zina vitu vinavyofanana. Na zote Dushelele na Kimbiji ni dance chotara (nyimbo za dance ambazo hazijakidhi viwango vya kuwa dance kamili). Ni nyimbo zinazojaribu kusikika kama za dance lakini hazikidhi viwango vingi vya kuwa nyimbo za dance kwakuwa kwanza zimepigwa kwa vyombo vichache na hivyo zinasikika zikipwaya masikioni,” niliandika kwenye sehemu ya maoni hayo.

Hivi karibuni nimekutana na Bob Junior ambaye aliyasoma maoni hayo na akatoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na wimbo huo.

“Ile nyimbo ni mchanganyiko wa ladha nyingi, kuna chakacha kuna mduara, kuna sebene na ndio maana ukaona mapigo yapo kama sebene na kuna magitaa. Gitaa ni live nimemwita mtu lakini mimi binafsi nilikuwa nahitaji ule muziki uwe vile, kama ningekuwa nahitaji sebene kabisa ningeita watu wa sebene. Lakini nimefanya iwe vile ili kwenye Bongo Flava iweze kupigwa na kwenye nyimbo ya sebene ipigwe. Lakini ningefanya moja kwa moja ingekuwa sebene, ingekuwa kwenye vipindi vya sebene,” amesema.

Msikilize zaidi Bob Junior hapa akiuelezea wimbo huo.

Related Articles

Back to top button