BurudaniPichaVideos

Exclusive interview na Amanda Swartbooi, model kwenye video ya Show Me ya Harmonize na Mavoko na Coolest Kids in Africa ya Davido

Amanda Swartbooi, ni sura ambayo utaiona sana mwaka huu. Macho ya wengi yalimuona mrembo huyu kwenye video ya Davido na Nasty C, Coolest Kids in Africa na hakika alionesha kuwa ni habari nyingine kwenye fani hiyo. Harmonize na Rich Mavoko wamefanikiwa kumtumia kwenye video ya wimbo wao, Show Me ambaye tayari ameifanya video hiyo iwe gumzo mtandaoni.

Nimemtafuta Amanda na kuzungumza naye mawili matatu ili kumfahamu zaidi. Fuatilia chat yetu hapo chini:

1. When did you start appearing on music videos?
Lini ulianza kuonekana kwenye video za muziki?

My first video was last year September 2016
Video yangu ya kwanza ilikuwa ni Septemba 2016

2. Is it something that you loved from before, or someone convinced you?
Ni kitu ambacho ulikuwa unapenda kufanya kabla ama kuna mtu alikushawishi?

The first video a friend asked me to help out .. after that video I decided to keep on doing it and pay for my studies

Video ya kwanza rafiki yangu aliniomba nisaidie, baada ya hapo niliamua kuendelea na kunisaidia kulipia masomo yangu

3. Apart from music videos, have you also done commercials?
Nje ya video za muziki, umeshafanya matangazo pia?

Yes I’ve only done one commercial

Ndio, nimefanya tangazo moja

4. What was your first music video?
Video yako ya kwanza ni ipi?

My first music video was FOUR4 by JR
Video yangu ya kwanza ilikuwa ni Four4 ya JR

5. How many videos have you appeared on, so far?
Umeonekana kwenye video ngapi hadi sasa?

In total I have done about 9 music videos and 8/9 I’m the main girl

Kwa ujumla nimefanya kama video 9 na 8 kati ya 9 mimi ni msichana mhusika mkuu

6. I think your breakthrough was when you appeared on Coolest Kid by Davido and Nasty C! How big was the the impact in your career?
Nadhani kutoka kwako ni pindi ulipoonekana kwenye wimbo Coolest Kid wa Davido and Nasty C! Hiyo imekuwa na mchango gani katika kazi yako?

The song had nothing special about it!. Most people watched the video because of me.So I’ll correct you there I had a huge impact on the song itself
Wimbo huo haukuwa na kitu chochote special. Watu wengi waliiangalia kwa sababu yangu. Kwahiyo ntakusahihisha hapo, mimi nilikuwa na mchango mkubwa kwenye wimbo wenyewe

7. How far can you go in a video, can lock lips with someone if a scene requires such thing?
Unaweza kufanya hadi nini kwenye video, unaweza kunyonyana ndimi na mtu kama scene inahitaji kitu kama hicho?

Most videos don’t want just a pretty girl. There has to be personality. Sometimes some serious acting.. but the most extreme is Kissing
Video nyingi hazijihitaji msichana mrembo peke yake. Lazima kuwe na personality. Wakati mwingine kuwepo na uigizaji wa uhakika, lakini zaidi sana labda kubusiana

8. Are your parents supportive?
Wazazi wako wanakuunga mkono?

Yes my parents support me through everything and anything..
Ndio, wazazi wangu wananiunga mkono kwenye kila kitu na chochote

9. Do you have a jealousy boyfriend? What are his views on your career?
Una mpenzi mwenye wivu? Vipi maoni yake kwenye kazi yako hii?

I am single
Nipo single

10. Here in Tanzania, people view video vixen as promiscuous, is it the same in South Africa?
Hapa Tanzania warembo wa video huonekana kama hawajatulia, Afrika Kusini iko hivi pia?

Yes and no .. In South Africa it isn’t Taboo anymore .. People will always have opinions regardless what your profession is .. but being a vixen is an art.. it is short term career and every woman that is part of this Should enjoy being sexy And make the most of it .. you only live once

Ndio na hapana. Hapa Afrika Kusini si kitu cha ajabu tena. Watu lazima watakuwa na la kusema bila kuzingatia kazi yako ni pia, lakini kuwa mrembo wa video ni sanaa, ni kazi ya muda mfupi na kila msichana ambaye ni sehemu yake lazima afurahie kuwa mrembo na kufanya kweli, unaishi mara moja tu.

11. How was it working with Rich Mavoko and Harmonize in Show Me?
Unazungumziaje kufanya kazi na Rich Mavoko na Harmonize kwenye Show Me?

Rich Mavoko and Harmonize are really cool ,down to earth people. They treated every woman on set with respect and it was an honor to work with them
Rich Mavoko na Harmonize ni watu poa sana, watu wazuri sana. Walimchukulia kila msichana kwenye video kwa adabu, ni heshima kufanya nao kazi

12. What do you think of Tanzanian music?
Unaounaje muziki wa Tanzania?

Tanzanian music is very calming and sensual
Muziki wa Tanzania ni wa kutulia na wenye hisia

13. Do you ever listen to any Tanzanian artist? If yes, who?
Unamsikiliza msanii yeyote wa Tanzania? Kama ndiyo, yupo?

I like Alikiba
Nampenda Alikiba

14. Harmonize posted you on his Instagram, do you get many Tanzanian followers now?
Harmonize amekupost kwenye Instagram, unapata followers wengi toka Tanzania sasa?

Yeah I got a few Tanzanian followers. (Ps I appreciate the love )
Ndio nimepata followers wachache wa Tanzania (Nashukuru kwa upendo)

15. What are three things that people don’t know about you?
Ni mambo gani matatu ambayo watu hawajui kuhusu wewe?

* I do my best in everything and anything I do. Whether it’s relationships or work
* I have a soft spot for animals
* I am a Libra : very calm.. love to make people laugh and spontaneous


*Najitahidi kufanya kwa ubora kwenye kila kitu na chochote ninachofanya, iwe uhusiano ama kazi
*Mimi ni muoga wa wanyama
*Mimi ni Mizani (nyota), mtulivu, napenda kuwachekesha watu na mtu wa uhalisia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents