Exim Bank Yaadhimisha Miaka 27 ya Kuwahudumia Watanzania
Benki ya Exim Tanzania imeadhimisha miaka27 tangu kuanzishwa kwake katika safari iliyojaa mafanikio, ubunifu, na huduma bora kwa wateja wake. Ikiwa na kaulimbiu‘Miaka 27 ya Kukupa Kipaumbele’, inaangazia mafanikio yakena mikakati madhubuti ambayo imejiwekea ili kuendelezamafanikio hayo miaka mingi ijayo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benkiya Exim Tanzania, Bw. Jaffari Matundu, alielezea baadhi yamafanikio makubwa ambayo benki imefikia tangu kuanzishwamwaka 1997.
“Miaka 27 iliyopita, tulianza safari ya kubadilisha sekta ya benkinchini na leo tunajivunia kuwa miongoni mwa watoa hudumabora wa kifedha. Mpaka sasa tumevuka mipaka tukiwa namatawi katika nchi tatu za Comoros, Djibouti, na Uganda,” alisema Matundu.
Dhamira ya Exim Bank ya ubunifu imekuwa nguzo kubwakatika mafanikio yake. Mfano, hivi karibuni, benki hiyoilitunukiwa tuzo ya “Chapa ya Benki Yenye Ubunifu Mkubwa Tanzania – 2024″ inayotolewa na jarida maarufu duniani la International Business Magazine ikiwa ni ushahidi wa hudumabora zinazotolewa na benki hiyo. Uboreshaji wa hivi karibuniwa mfumo wake wa Kibenki (CBS) ni sehemu ya mikakati yaExim Bank kuboresha na kuongeza uharaka wa miamala, usahihi, na huduma bora kwa wateja kiujumla.
Mwaka 2023, Benki ya Exim ilipata mafanikio makubwa yakifedha, ikiwa na faida kabla ya kodi ya TZS bilioni 91.5, uwekaji wa fedha za Wateja kufikia TZS trilioni 2.4, na jumla yamali ikivuka TZS trilioni 3. Mafanikio haya yanaoneshakiwango cha uaminifu wa benki ya Exim kwa wafanyakazi naimani kwa wateja wake.
Benki ya Exim itaendelea kukua na kujipambanua zaidikuongeza wigo na kufikia maeneo zaidi ndani na nje yaTanzania. “Tutaendelea kuwa wabunifu, kutafuta namna bora zaidi za kutoa huduma kwa wateja wetu na hivyo kuchangiakatika maendeleo ya sekta ya kifedha. Tuna malengo yakuboresha ufanisi wa utendaji wetu, huduma kwa wateja, nabidhaa tunazotoa, kuhakikisha Exim Bank inaendelea kuwakinara katika sekta ya kibenki nchini,“ aliongeza Matundu.
Stanley Kafo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano waExim Bank, akielezea kuhusu safari yao, “Tunajivunia timu yetukwa kazi nzuri na wateja wetu wote. Ni jambo la faraja kujuakwamba tunachangia katika ukuaji na kuboresha maisha yaWatanzania kote nchini.”
Benki ya Exim inaposherehekea mafanikio haya, Matundu alitoashukrani kwa wateja, wanahisa, wafanyakazi, na washirika wabenki hiyo. “Msaada wenu kila wakati umechangia katikamafanikio haya. Tunahaidi kuendeleza safari yetu ya ubora, ubunifu, na ukuaji, kuhakikisha Benki ya Exim inabaki kuwamstari wa mbele katika sekta ya benki nchini,” alihitimisha.