Michezo

Fahamu alichosema, Mukoko Tonombe kuhusu ubingwa

Kiungo fundi wa Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Mukoko Tonombe amesema kuwa tangu Ligi Kuu msimu huu ilivyoanza mpaka sasa wanacheza vizuri na wamechukua wachezaji wazuri.

Mukoko ameyasema hayo wakati alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Mwanaspoti huku akiongeza kuwa wanachohitaji kuona Ligi inakwisha vizuri.

”Tunataka ligi iishe vizuri tuchukue kombe, tangu Ligi imeanza mpaka sasa hivi tunacheza vizuri, tunachukua wachezaji wazuri, tumeanza Ligi vizuri mpaka sasa hivi watu wanaona tunakwenda vizuri, tunataka kuangalia mpaka Ligi itakapokwisha.”- Mukoko

Yanga SC kwa sasa ipo jijini Arusha kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania siku ya Jumapili.

Related Articles

Back to top button