Fahamu: Bustani ya Maajabu jijini Dubai

Jiji la Dubai, lililopo katika nchi ya Falme za Kiarabu, linafahamika kwa maajabu mengi ikiwemo jengo refu kuliko zote duniani, lakini kati ya maajabu yanayostaajabisha ni hili linalofahamika kama ‘Dubai Miracle Garden’.

Bustani ya Dubai Miracle Garden, ni bustani ya maua iliyokaa kwenye mita za mraba 72,000 za ardhi, na kusheheni maua zaidi ya milioni 150. Dubai Miracle Garden ilizinduliwa mwaka 2013 katika siku ya wapendanao.

Bustani hii ndio kubwa kuliko zote duniani na imeshikilia rekodi ya Dunia ya Guiness kwa mwaka 2013, 2016 na 2018.

Ingawa Jiji la Dubai, linafahamika kwa hali ya hewa yenye joto Sana kipindi cha kiangazi , uwezo wa bustani hii kustahimili joto unatokana na mfumo wa umwagiliaji unaojulikana kama drip irrigation.

Inasadikika kwamba bustani hii hutumia zaidi ya lita laki saba na hamsini na saba elfu kila siku. Maji hayo hupatikana katika maji yanayotumika na wakazi wa Jiji la Dubai,  na kisha kutibiwa na kutumika tena kuyamwagilia maua.

 

Karibu Dubai? utembelee bustani hii ya maajabu.

SHIRIKA la Ndege la Emirates huendesha safari zake mara tatu kwa wiki kati ya Dar Es Salaam na Dubai.

 

 

Related Articles

Back to top button