Siasa

Fahamu changamoto alizokutana nazo Biden wakati anakabidhiwa ‘Black Box’ Sanduku la nyuklia na Trump (+ Video)

Ni mojawapo ya matukio ambayo hayakuangaziwa hadharani , lakini ni muhimu katika hatua ya rais mmoja kumkabidhi mamlaka rais mpya nchini Marekani.

Kwa miongo sita sasa, wakati wa kuapishwa kwa rais mpya Januari 20, hafla inayofichwa na shamrashamra zinazoendelea, wanajeshi wawili waliovalia sare zao za kijeshi wamekuwa wakisubiri kandokando wakati wa muda wa kuapishwa.

Mmoja wao , ambaye huandamana na rais anayeondoka mamlakani katika safari zake nyingi , hubeba sanduku zito ambalo humkabidhi afisa mwingine ambaye atakuwa akiandamana na rais huyo mpya .

Sanduku hili ndilo inaloitwa black Box ama ‘sanduku la nyuklia’, sanduku lililotengenezwa kwa chuma linalomuandama rais wa Marekani kila mahali iwapo anataka kurusha bomu la kinyuklia akiwa nje ya ofisi.

Tangu sanduku hilo lilipoanza kutumika wakati wa utawala wa rais John F Kennedy, ubebaji wa sanduku hilo umekuwa kitu muhimu licha ya kutokuwa miongoni mwa vitu muhimu katika sherehe hiyo ya kumuapisha rais mpya nchini Marekani.

Hatahivyo , mwaka huu njia rahisi ya kukabidhi sanduku hilo kutoka mkono mmoja hadi mwingine ilikabiliwa na changamoto kubwa : kwa mara ya kwanza katika zaidi ya karne moja, rais anayeondoka mamlakani hakuwepo katika halfa ya kumuapisha mrithi wake.

Kulingana na itifaki , Trump alipaswa kuwa na sanduku hilo la nyuklia hadi saa sita .

lakini kufikia wakati huo tayari alikuwa umbali wa kilomita 1500, kusini mwa Florida mbali na rais Biden , ambaye alipaswa kumkaribisha wakati huo.

Hatahivyo kuna masunduku kama hayo kulingana na watalaamu ambayo huwa tayari kutumika katika matukio kama hayo.

Hivyobasi tunauliza je hafla hiyo ya kukabidhiana sanduku hilo la kinyuklia inafanyika vipi iwapo marais hao walikuwa maeneo tofauti?

Suluhu isiyo ya kawaida

Ikiwa na wasiwasi ya jinsi sanduku hilo la nyuklia lingekabidhiwa utawala wa Biden , Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon hivi majuzi ilijibu kwamba ilikuwa na mpango wa siku ya kuapishwa kwa rais mpya, lakini ikakataa kutoa maelezo.

Hatahivyo , wataalam kadhaa na wasomi walielezea matukio kadhaa yanayoweza kufanyika iwapo hali hiyo isiyo ya kawaida itafikia hapo katika historia ya Marekani .

Wakati wa hafla ya kituo cha udhibiti wa silaha, Stephen Schwartz, alielezea kwamba tofauti na fikra za wengi kuna masunduku matatu ya aina hiyo.

Moja ni lile linaloandamana na rais , lakini kuna orodha nyingine ya dharura inayopewa makamu wa rais ama mtu aliyepona { waziri ambaye huteuliwa kuchukua mamlaka iwapo kwa sababu fulani viongozi wote wamefariki}

Schwartz alisema kwamba Pentagon inaweza kutumia mojawapo ya masunduku yake – ama kuandaa jipya ili kumkabidhi Biden na kulifanya kuweza kufanya kazi punde Biden atakapoapishwa.

Mara nyingi, sanduku hilo haliwi mbali na Rais wa Marekani

Wakati huo , usimamizi wa Trump wa nyuklia na udhibiti unaisha , hivyobasi kadi zake zinazotoa nambari hizo za siri za sanduku hilo la nyuklia huzimwa.

“Iwapo afisa anayebeba sanduku hilo ataandamana na Trump katika ndege ya Airforce One kuelekea Florida , msaidizi huyo ataondoka mahala alipo Trump mwendo wa saa sita kamili na kurudi Washington na sanduku hilo, Schwartz aliambia CNN.

Mchakato halisi

Ni hali hiyo ambayo suala la sanduku hilo limezua maswali mengi na matumizi yake yamewavutia mamilioni ya watu miaka yote.

Hatahivyo kile ambacho watu hawakijui ni kwamba nambari za siri na funguo zake katika sanduku hilo ambazo zinamruhusu rais kuwa na uwezo wa kutoa maagizo ya kutekeleza shambulio hazipo katika sanduku hilo.

Funguo hizo za uwezo wa kutekeleza shambulio la kinyuklia huwa ni kadi ndogo ya plastiki ambayo rais aliye madarakani hubeba mfukoni. Kadi hiyo hujulikana kama ”Code of Gold au Cookie”

Rais hutakiwa kuikata mara mbili ili kuthibitisha utambulisho wake anapowasiliana na kitengo cha vita katika Pentagon , ili kuruhusu shambulio.

Mapema siku ya kuapishwa kwa rais , rais mpya na makamu wake hupokea maagizo ya jinsi ya kutumia sanduku hilo na rais anayechukua mamlaka hupatiwa kadi hiyo.

Kulingana na jarida la sayansi ya atomiki , Pentagon huzima kadi ya rais anayeondoka madarakani saa sita siku ya kuapishwa kwa rais mpya huku kadi ya rais mpya ikiwashwa.

Hivyobasi saa sita na dakika moja Januari 20, kwa mfano iwapo Trump angetaka kutekeleza shambulio la kinyuklia , asingeweza kufanya hivyo, iwapo bado alikuwa anamiliki sanduku hilo na Biden naye hangeweza kufanya hivyo saa tano na dakika 59 asubuhi.

Hofu kwamba Trump angetekeleza shambulio la nyuklia kabla ya kuondoka kwake katika serikali ilizua wasiwasi kufuatia ghasia za uvamizi wa jengo la bunge la Capitol Hill mapema mwezi huu.

Wakati huo kiongozi wa bunge hilo Nancy Pelosi , aliwasiliana na idara ya ulinzi na kuwataka kutofuata maagizo ya Trump iwapo angetaka kutekeleza shambulio hilo kabla ya kuondoka katika ikulu ya White House.

Sanduku

Bruce Blair, mwanachama mstaafu wa kundi la timu ya kutekeleza shambulio la nyuklia nchini Marekani , awali alielezea BBC , kwamba tofauti na jinsi watu wanavyoamini, sanduku hilo la Nyuklia halina kitufe ama nambari za siri zinazomwezesha rais kutekeleza shambulio la nyuklia moja kwa moja , na badala yake itifaki za shambulio hilo ni sharti awasiliane na washauri wa ngazi za juu.

“Katika sanduku hilo pia kuna mchoro wa mpango wa vita , malengo yake pamoja na idadi ya watakaofariki bila kusahau silaha zilizopo.

”Hivyobasi ni rahisi kuelewa hali ilivyo katika sekunde chache”, alisema Blair.

Kuapishwa kwa Biden kumekuwa kwa tofauti kama ilivyozoeleka kwa mujibu wa desturi, ikiwemo kukabidhiwa sanduku la nyuklia

Ndani ya sanduku hilo si nambari za siri pekee za kutekeleza shambuliko hilo la uharibifu , pia kuna vitabu viwili.

Kimoja kina maelezo ya kina kuhusu aina ya shambulio hilo la nyuklia ambalo linaweza kutekelezwa na orodha nyingine ya maeneo salama kwa rais wa Marekani na familia yake kujificha.

Wakati mwingi sanduku hilo huonekana na antena iliojitokeza ambayo hutumika kuimarisha mawasiliano ya moja kwa moja na idara ya ulinzi The Pentagon.

Bofya hapa kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CMEsZkBBn6q/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents