Habari

Fahamu kinachoendelea Guinea, utawala wa kijeshi na hatma ya uchaguzi

Watawala wa kijeshi nchini Guinea jana wameondoa uwezekano wa kumruhusu rais wa zamani anaeshikiliwa Alpha Conde kwenda uhamishoni, na kusema mchakato wa mpito kuelekea utawala wa raia utafanyika kulingana na matakwa ya raia wa nchi hiyo.

Guinea refuses to allow deposed president to leave the country | Alpha  Conde News | Al Jazeera

Taarifa ya baraza la uongozi huo, imetolewa katika kukaidi shinikizo la kimataifa la kuachiwa huru Conde na kuwasilisha ratiba ya miezi sita ya kuandaliwa kwa uchaguzi, baada ya mapinduzi ya Septemba 5 kuibua ukosoaji wa kimataifa.

Katika mkutano wa kwanza wa baraza hilo la uongozi na wanahabari kuhusu muda wa mwisho wa miezi sita wa kuandaliwa kwa uchaguzi, msemaji wake kanali Amara Camara amesema kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo Mamady Doumbouya ameuambia ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS unaozuru nchini humo kwamba ni muhimu kwa Jumuiya hiyo kusikiliza matarajio halali ya watu wa Guinea na kwamba ipo haja ya kutorudia makosa ya zamani huku akisema kwamba mashauriano ya kitaifa ya kuleta mabadiliko yalianza siku ya Jumanne na ni raia huru wa Guinea watakaoamua hatima yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents