Fahamu

Fahamu kiundani kuhusu jengo la ghorofa 70 litakalojengwa Zanzibar

Jengo la ghorofa 70, urefu wa mita 385 litakalojengwa Zanzibar katika kisiwa cha Chapwani Unguja litakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo maeneo ya biashara na hoteli na jumla ya dola za Marekani Bil.1.3 zimetengwa kwa ajili ya hatua za awali na linatarajiwa kukamilika baaada ya miaka minne.

Jengo hilo la kibiashara litakapokamilika litaitwa Zanzibar Domino Commercial Tower, na litajengwa umbali wa kilometa 15 kutoka Mji Mkongwe katika eneo la hekta 20 ambapo pamoja na mambo mengine litakuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano utakaobeba watu 1,000 na Jengo la namna hiyo pia litakuwa la kwanza Afrika Mashariki na Kati.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa makubaliano baina ya kampuni ya Kitanzania ya AICL Group na kampuni ya XCassia yenye utaalamu na uzoefu wa kusanifu na kuchora ramani za majengo marefu duniani kupitia uongozi wa Edinburg Crowland Management Ltd yenye ofisi zake katika majiji ya New York na Dubai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents