Fahamu

Fahamu kiundani sababu ya vita ya Wapalestina na Waisrael, sababu za kidini zahusishwa na mji wa Jerusalem (+ Video)

Ukijulikana kiHebrew kama Yerushalayim na kiarabu kama Al Quds, ni mmoja wa miji ya zamani zaidi duniani.

Umetekwa, kuharibiwa na kujengwa kwa mara nyengine ,na kila safu ya dunia kipande tofauti cha historia yake hubainika.

Ijapokuwa mji huo umezongwa na hadithi za tofauti na mizozo kati ya watu wa dini tofauti, huunganishwa na heshima ya mji huo mtakatifu.

Wayahudi na Waislamu katika lango la Damscus mjini Jerusalem
Wayahudi na Waislamu katika lango la Damscus mjini Jerusalem

Katikati yake ni mji wa zamani , uliosheheni historia unaoelezea majirani zake wane : Wakristo, Waislamu Wayahudi na Warmenia.

Mji huo umezungukwa na ukuta wenye mawe na ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo takatifu zaidi duniani.

Jerusalem ni mojawapo ya maeneo yanayozozaniwa sana duniani
Jerusalem ni mojawapo ya maeneo yanayozozaniwa sana duniani

Kila eneo jirani linawakilisha idadi yake ya watu. Wakristo wana maeneo mawili, kwasababu Warmenia pia ni Wakristo na ujirani wao ukiwa mdogo zaidi kati ya maeneo hayo manne, ni moja ya kituo cha zamani zaidi cha Armenia duniani. Ni wa aina yake kwasababu jamii hiyo imehifadhi utamaduni wake ndani ya hekalu.

Sababu kubwa ni hizi tatu.

1.Kanisa la mtakatifu Sepulcher.

2.Msikiti wa Al Aqsa.

3. Ukuta wa Kotel. Western Wall

Fuatilia video hii chini kufahamu kiundani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents