Habari

Fahamu kuhusu uhaba wa bidhaa ya maziwa ya watoto Marekani

Ndege za kwanza zilizobeba maziwa ya watoto kutoka Ulaya, zilizoidhinishwa na Rais Joe Biden kusaidia kuleta nafuu kwa  upungufu mkubwa wa bidhaa hiyo Marekani, zitawasili huko Indiana katika ndege ya kijeshi wikiendi hii, White House ilitangaza Ijumaa.

White House imesema shehena 132 za maziwa ya watoto aina ya Nestle Health Science Alfamino na nyingine ya Alfamino Junior formula zitasafirishwa kutoka kituo cha jeshi la anga cha Ramstein Ujerumani na kuwasili Marekani wikiendi hii.

Shehena 114 nyingine ya maziwa aina ya Gerber Good Start Extensive HA formula zinatarajiwa kuwasili katika siku zijazo. Kwa jumla takriban chupa milioni 1.5 za aunsi 8 za aina tatu za maziwa ya watoto, ambayo hayana madhara kwa watoto wenye kudhurika na proteni ya maziwa ya ng’ombe, zitawasili wikiendi hii.

Wakati Biden awali aliiomba Wizara ya Ulinzi kutumia ndege za biashara za kukodi kusafirisha maziwa hayo ya makopo kutoka Ulaya kuja Marekani, White House imesema kulikuwa hakuna ndege za biashara mwishoni mwa wiki. Badala yake, ndege za jeshi la anga zitasafirisha shehena ya kwanza ya maziwa hayo.

Utawala wa Biden umeziita juhudi hizo “Operesheni ya Fly Formula,” wakati ikijitahidi kutatua uhaba wa maziwa nchi nzima, hususan aina mbalimbali za maziwa yasiyokuwa na madhara kwa watoto, baada ya kufungwa kwa kiwanda cha kutengeneza maziwa ya watoto kikubwa kuliko vyote nchini mwezi Februari kwa sababu za kiusalama.

Wadhibiti na watengenezaji wa Marekani, Abbott, wana matumaini ya kufunguliwa tena kiwanda cha Michigan, lakini itachukuwa takriban miezi miwili kabla ya bidhaa hiyo kuwa tayari kufikishwa sokoni.

Idara ya Usimamizi wa Chakula na Dawa wiki hii ililegeza masharti ya uagizaji wa maziwa ya watoto ya makopo ili kupunguza makali ya usambazaji wa bidhaa hiyo, ambayo imeyaacha maduka yakiwa hayana baadhi ya aina hiyo ya maziwa na maduka ya rejareja kudhibiti usambazaji wa bidhaa hiyo kwa wazazi wenye wasiwasi kuwapa maziwa hayo watoto wao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents