Bongo5 ExclusivesFahamuHabariLifestyleMichezo

Fahamu Mo Salah anavyowathamini watu kijijini kwao Nagrig, analipa masikini kila mwezi

Mshambuliji wa klabu ya Liverpoo Mohamed Salah amekuwa mfano mzuri w akuigwa kwa namna anavyojaribu kubadilisha kiji alipozaliwa huko nchini Misri.

Kijiji hicho kinachojulikana kwa jina la Nagrig nchini Misri kipo umbali wa kilometa 124.2 kutoka Kaskazini mwa jiji la Cairo.

Ikumbukwe Salah sio mzaliwa wa Cairo wala majiji makubwa misri kama Cairo, Alexandria, Salah inaelezwa kuwa katika kijiji chao amejenga hospitali, shule, kituo cha vijana cha michezo na kitengo cha magari ya wagonjwa kwa watu wake katika kijiji chake.

Mbali na hilo Salah amejenga kituo cha kuratibu maji safi kinachoelezwa kugharimu $450,000 sawa na T sh 1,049,400,000/= ili kutoa maji ya kunywa kwa watu wake.

Kubwa zaidi Salah anatoa £3,500 sawa na Tsh 8,162,000 kwa familia maskini kila mwezi katika kijiji chake.

Put some respect kwa Legend huyo wa Misri kutoka katika kijiji cha Nagrig.

Related Articles

Back to top button