Fahamu namna baadhi ya kampuni zinavyosaidia watu kutoweka

Kote duniani, kuanzia Marekani, Ujerumani hadi Uingereza, baadhi ya watu huamua kutoweka na kuanza maisha mapya mahali wasipojilikana na mtu yeyote – wakiacha nyuma familia zao.

Nchini Japan, watu hawa wanafahamika kama “jouhatsu”. Hili ni neno la Kijapani linalomaanisha “kutoweka kama mvuke “,lakini pia linatumika kuashiria watu wanaotoweka kwa sabau maalumna wanaendelea kujificha wasijulikane walipo -kwa miaka au miongo kadhaa.

“Nilichoshwa na mahusiano yangu. nikaamua kukusanya virago vyangu na kutoweka,” anasea Sugimoto,42, ambaye anatumia jina la familia kwa ajili ya taarifa hii. “Niliamua kupotea tu.”

Anasema katika kijiji chao kila mtu alikuwa anamjua kwa sababu familia yake ilikuwa maarufu kutokana na biashara iliyokuwa ikiendesha na Sugimoto alitaraiwa kuiendeleza.

Lakini kutokana na majukumu aliyopewa na ambayo yalikuwa yakimtatiza kimawazo aliamua kutoroka nyumbani na hakuna mtu anyejua alipo.

Streets in Japan
Mwanasosholojia Hiroki Nakamori amekuwa akifanya utafiti juu ya jouhatsu kwa zaidi ya muongo mmoja

Kuanzia visa vya kuzongwa na madeni na ndoa zisizo na mapenzi ndio baadhi ya vitu ambavyo vinawafanya jouhatsu “kupotea”.

Licha ya sababu walizo nazo, wanageukia makampuni yanayowasaisia katika mchakato huo. Oparesheni yenyewe inafahamika kama “huduma ya kuhama usiku”, kutokana na usiri unaohusishwa na kuwa jouhatsu. Wanasaidia watu wanaotaka kupotea kimya kimya kuhama kisiris, na pia wanaweza kuwapatia makao katika maeneo ya kisiri.

“Mara nyingi, sababu ya kuhama huwa ni jambo zuri kama kujiunga na chuo kikuu, ajira aua ndoa.

“Lakini pia kuna kuhama kwa ubaya – kwa mfano kuachana na masoma chuo kikuu, kupoteza kazi au kutoroka mtu anayekufuatilia,” anasema Sho Hatori,ambaye ni muanzilishi wa kampuni ya kuhama usiku miaka ya 90 wakati gharama ya maisha ilipopanda kupita kiasi nchini Japan.

Mwanzoni ilidhaniwa sababu za kiuchumi ndio sababu pekee inayowafanya watu kutoroka lakini baadae aligundua kuna “sababu za kijamii”, pia. “Alichofanya ni kuwasaidia watu kuanza upya maisha mara ya pili,” anasema.

Mwanasosholojia Hiroki Nakamoriamekuwa akifanya utafiti juu ya jouhatsu kwa zaidi ya muongo mmoja.Anasema neno ‘jouhatsu’ kwanza lilianza kutumiwa kuelezea watu ambao waliamua kupotea katika miaka ya 60.

Maisha ya pili

Viwango vya talaka vilikuwa (na bado) viko chini sana Japan, Kwa hivyo ilikuwa rahisi kwa watu kuondoka na kuwaacha wenza wao badala ya kupitia mchakato mrefu wa talaka rasmi.

Mwanamke akitoa pesa katika ATM
Nchini Japan ni rahisi kwa mtu aliyepotea kufikia fedha zake bila kuwajulisha wale ambao huenda wanamtafuta

“Nchi Japan, ni rahisi sana kutoweka usiowahi kuonekana tena,” anasema Nakamori. Taarifa binafsi za watu zinalindwa kikamilifu: Kiasi kwamba watu waliopotea wanaweza kutoa pesa katika akaunti zao za benki kupitia mitambo ya ATM bila kuwa na hofu ya kujulikana na familia zao haziwezi kufikia video za usalama ambazo huenda zimewanasa wapendwa wao waliotoweka.

“Polisi haiwezi kuingilia kati mpaka kuwe na sababu nyingine – kama uhalifu au ajali. Kile ambacho familia inaweza kufanya nikulipa wapelelezi wengi wa kibinafsi au wasubiri. Hiyo ndio njia pekee.”

Nilishtuka sana

Kwa jamaa walioachwa nyuma na wapendwa wao – hofu ya kuwatafuta jouhatsu wao – inaweza kuwaathiri vibaya.

“Nilishtuka sana,” anasema mwanamke ambaye hakutajwa jina, na ambaye mwanawe wa kiume wa miaka 22- alitoweka na hajawahi kuwasiliana naye.

“Hakufaulu baada ya kuacha kazi mara mbili. Lazima ailijihisi vibaya kwa kufeli.” Alisafiri hadi mahali anakoishi, kupekuwa nyumba hiyo na kusubiri kwenye gari kwa siku kadhaa lakini hakurudi. Hakuwahi kurudi.

Anasema polisi hawajamsaidia, walimwambia wanaweza tu kuingilia kati wakishuku huenda kuna uwezekano wa kujitoa uhai. Lakini kwa kuwa hakuna kijikaratasi kilichoachwa nyuma, hawawezi kusaidia.

“Naelewa kuna watu wanaomfuatilia mtu – taarifa zinaweza kutumiwa vibaya. Hii ni sheria muhimu, pengine. Lakini wahalifu na wazazi hawawezi kuwatafuta watoto wao pia? Wote wanachukuliwa sawa kwa kuwa wanalindwa. Hii ni nini sasa?” alisema.

“Sheria tuliyonayo sasa, bila pesa, kile ninachoweza kufanya ni kutafuta [a] mwili wa mwanangu- ndio kitu pekee ninachoweza kufanya.”

Waliopotea

A woman in Tokyo
The police rarely help families searching for their loved ones

Kwa jouhatsu wenyewe, hisia ya masikitiko na kujutia kitendo walichofanya huwaathiri wengi wao hata baada ya kuondoka na kwenda kwengine kuanza maisha mapya.

“Muda wote nahisi nimefanya makosa,” anasema Sugimoto, mwanabiashara aliyeondoka na kumuacha mke wake na watoto.

“Sijawaona [watoto wangu] kwa mwaka mmoja sasa. Niliwaambia niko safari ya kikazi.”

Anachojuti zaidi, anasema, ni kuwaacha. Sugimoto kwa sasa anaishi eneo la makazinje kidogo ya mji wa Tokyo.

Tokyo
Tokyo ni moja ya miji mikubwa duniani, ikiwa na jumla ya wakazi milioni 37

Kampuni iliyomsaidia kupotea inaendeshwa na mwanamke anayefahamika kama Saita, ambaye pia hatumii jina la familia ili kulinda utambulisho. Yeye mwenyewe pia alikuwa jouhatsu aliyetoweka kwao miaka 17 iliyopita.

Aliamua ‘kupotea’ baada ya kuwa katika uhusiano mbaya, anasema “kwa njia fulani, mimi ni mtu aliyepotea – mapaka sasa jamaa zangu hawajui nilipo.”

“Nina wateja aina tofauti,” anaendelea kusema. “kuna watu wanaotoroka dhulma za kinyumbani au sababu za kibinafsi. Simhukumu mtu. Wala sisemi, ‘Sababu yako ina uzito’.Kila mtu nakabiliwa na changamoto binafsi maishani.”

Related Articles

Back to top button