Fahamu

Fahamu namna Marekani inavyoisaidia Israel kwenye mzozo na Palestina, kiasi cha fedha kinachotoka

Kufuatia kuongezeka kwa ghasia za hivi karibuni kati ya Waisraeli na Wapalestina, Rais Joe Biden anakabiliwa na maswali kutoka kwa wanachama wa chama chake cha Democratic kuhusu kiwango cha misaada ambacho Marekani hutuma kwa Israel.

Seneta Bernie Sanders alisema Marekani lazima “iangalie sana” namna pesa zinavyotumiwa. Hivyo basi Israeli hupata fedha kiasi gani kutoka Washington na huitumia kwa shughuli gani?

Kiasi gani cha msaada Marekani hukitoa?

Mnamo mwaka wa 2020, Marekani ilitoa msaada wa dola bilioni 3.8 kwa Israel kama sehemu ya ahadi ya kila mwaka ya muda mrefu iliyofanywa chini ya utawala wa Barack Obama. Karibu misaada hii yote ilikuwa kwa ajili ya msaada wa kijeshi.

Mkataba uliosainiwa mnamo 2016 na Rais Obama unaangazia jumla ya dola za Marekani milioni 38.000 za msaada wa kijeshi kwa muongo mmoja wa mwaka 2017-2028.

Kwa kuongezea hili, mwaka jana Marekani ilitoa dola za Kimarekani milioni 5 kuwapa makazi wahamiaji nchini Israel. Nchi hiyo ina sera ya kukubali Wayahudi kutoka sehemu nyingine za ulimwengu kama raia.

Israel imetumiaje fedha za Marekani?

Kwa miaka mingi, pesa kutoka Marekani zilisaidia Israel kukuza moja ya majeshi yaliyoendelea zaidi ulimwenguni, na pesa hizo zinasaidia kununua vifaa vya kisasa vya jeshi la Marekani.

Kwa mfano, Israel ilipata ndege 50 za kivita za F-35, ambazo zinaweza kutumika kwa mashambulizi ya kombora. Kufikia sasa ndege 27 zimeshafikishwa, kwa gharama ya karibu Dola za Marekani milioni 100 kila moja.

Mwaka jana, Israel pia ilinunua ndege nane za KC-46A Boeing Pegasus kwa wastani wa dola bilioni 2.4. Hizi zina uwezo wa kuongeza mafuta kwenye ndege kama F-35 angani.

Tangu vita vya pili vya dunia, Israel imekuwa ndiye mpokeaji mkubwa zaidi wa misaada ya nje ya Marekani

Kati ya dola bilioni 3.8 zilizopewa Israeli mnamo 2020, dola milioni 500 zilikuwa kwa ajili ya ulinzi wa makombora, ambayo ni pamoja na uwekezaji katika mifumo mingine ambayo inaweza kuzidhibiti roketi zinazoingia kwa mashambulizi.

Tangu 2011, Marekani imechangia jumla ya dola bilioni 1.6 kwa mfumo wa ulinzi wa Iron Dome.

Namna mfumo wa Iron Dome unavyofanya kazi

Kwa kuongezea, Israel ilitumia mamilioni kushirikiana na Marekani kwa maendeleo ya teknolojia ya kijeshi, kama mfumo wa kugundua mashimo ya chini ya ardhi yaliyotumiwa kupenya Israel.

Serikali ya Israel inawekeza sana katika vifaa vya kijeshi na mafunzo, na hutumia misaada kutoa ujumbe kwamba si nchi ndogo kuliko mataifa mengine yenye nguvu.

Inafanishwa vipi na nchi nyingine?

Tangu vita vya pili vya dunia, Israel imekuwa ndiye mpokeaji mkubwa zaidi wa misaada ya nje ya Marekani.

Mnamo mwaka wa 2019, mwaka wa hivi karibuni kuchapisha takwimu kamili, Israel ilikuwa mpokeaji wa pili kwa ukubwa wa misaada ya kigeni ya Marekani baada ya Afghanistan, kulingana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

Pesa nyingi zilizotolewa kwa Afghanistan zilitumika kuunga mkono juhudi za jeshi la Marekani la kutuliza nchi hiyo, iliyokuwa katika vita wakati wa uvamizi wa Marekani mnamo mwaka 2001

Lakini kwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, iliyopangwa kufanyika Septemba mwaka huu, karibu dola milioni 370 tu ziliombwa kufikia mwaka 2021.

Israeli inapokea pesa nyingi zaidi katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Misri na Jordan pia ni wapokeaji wakuu wa misaada ya Marekani. Wote wawili wana mikataba yao ya amani na Israel.

Kila mmoja alipokea karibu Dola za Marekani milioni 1.5 za msaada mnamo mwaka 2019.

Wakati huo huo, Rais Biden alirudisha pesa kiasi cha dola milioni 235 kwa shirika la UN linalosaidia wakimbizi wa Kipalestina. Fedha hii ilikatwa na serikali ya mtangulizi wake, Donald Trump, mnamo 2018.

Kwanini Marekani inatoa msaada mwingi kwa Israel?

Kuna sababu kadhaa kwa nini Marekani inatoa msaada mwingi kwa Israel, pamoja na ahadi za kihistoria zinazohusiana na msaada wa Washington kwa kuundwa kwa serikali ya Kiyahudi mnamo 1948.

Kwa kuongezea, Israel inachukuliwa na Marekani kama mshirika muhimu katika Mashariki ya Kati, na malengo ya pamoja na kujitolea kwa pande zote kwa maadili ya kidemokrasia.

“Misaada ya nje ya Marekani imekuwa sehemu muhimu katika kuimarisha uhusiano huu,” inasema idara ya Utafiti ya Congress.

“Maafisa wa Marekani na wabunge wengi kwa muda mrefu wamekuwa wakiitazama Israel kama mshirika muhimu katika eneo hilo.”

Rais Joe Biden anakabiliwa na maswali kutoka kwa wanachama wa chama chake cha Democratic kuhusu kiwango cha misaada ambacho Marekani hutuma kwa Israel.

“Msaada wa Marekani husaidia kuhakikisha kuwa Israel inaimarisha jeshi lake dhidi ya vitisho vya kieneo,” linasema shirika la usaidizi wa kigeni la Marekani.

Na “inalenga kuhakikisha kuwa Israel iko salama vya kutosha kuchukua hatua za kihistoria zinazohitajika kufikia makubaliano ya amani na Wapalestina na kwa amani kamili ya kikanda.”

Kuhakikisha kuwa Israel inaweza kujilinda dhidi ya vitisho katika ukanda imekuwa msingi wa sera za kigeni za Marekani kwa marais wote wa Democratic and Republican kwa miongo kadhaa.

Jukwaa la uchaguzi la Chama cha Democratic la mwaka 2020 lilielezea “msaada mkubwa” kwa Israel, lakini wengine kwenye mrengo wa kushoto zaidi wa chama sasa wanahoji ahadi ya misaada ya Marekani kwa nchi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents