Michezo

Fahamu sababu ya Ronaldo kutohudhuria tuzo za FIFA jana, atumia usiku huo kuwa na familia nakuandika ujumbe huu

Hapo jana siku ya Jumatatu kulikuwa na usiku wa tuzo ambapo kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa soka ulimwenguni waliweza kushuhudia baadhi ya watu wakifanikiwa kuondoka na tuzo huku macho na masikio ya walio wengi yalikuwa yakiangazia kwa nafasi ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA 2019 kipengele ambacho kinawakutanisha mahasimu wawili na wanasoka bora na vipenzi wa mashabiki Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ukiachia mbali Virgil van Dijk akiwemo kwenye kipengele hicho.

https://www.instagram.com/p/B2xFV0PAF6a/

Katika usiku huo maalum ambao ulihudhuriwa na wanasoka mbalimbali ulishuhudiwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA 2019 na kumpiku beki wa Liverpool, Virgil van Dijk pamoja na hasimu wake Ronaldo.

Mbali na wachezaji waliyokuwepo kwenye orodha ya kuwania tuzo hizo kuwasili katika jiji la Milan nchini Italia ili kuhudhuria tukio hilo hali ilikuwa ni tofauti kabisa na nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo kwani yeye alikuwa  nyumbani kwake usiku huo akipumzika na familia yake.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kufanyika kwa tukio hilo kocha wa klabu ya Juventus, Maurizio Sarri alisema kuwa mchezaji wake raia wa Ureno, Ronaldo amepata majeraha na kupelekea hata kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha leo ktakacho ikabili Brescia.

“Nitaangalia mabadiliko gani nitakayofanya, jana Ronaldo alipata majeraha lakini ni kawaida kwa wachezaji maana alicheza dakika nyingi,” amesema Sarri.

Ronaldo aliposti picha usiku huo kupitia akaunti yake ya Instagram inayomuonesha akiwa nyumbani kwake akijisomea kitabu huku akiandika ”Uvumilivu na kutokukata tamaa ni sifa mbili ambazo zinazomtofautisha mtu ‘professional na amateur’.”

Messi ulikuwa usiku wa fura mno kwa upande wake baada ya kutwaa tujzo hiyo hasa kutona na kazi kubwa aliyofanya msimu uliyopita wa 2018/19 akifunga jumla ya mabao 54 kwenye michezo 58 aliyocheza na kutoa pasi za mwisho 20 zilizochangia kupatikana kwa magoli.

Hata hivyo Ronaldo mwenye miaka 34, amefunga jumla ya magoli 31 katika michezo 47 aliyocheza msimu uliyomalizika wa mwaka 2018/19.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents