Michezo

Fahamu sheria maalum za AFCON chini ya janga la Corona, idadi ya wachezaji na mengineyo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika lazima zicheze mechi zake ikiwa angalau wachezaji wao 11 wamepimwa na kukutwa hawana maambukizi ya COVID-19, waandalizi wa mashindano wamesema.

Endapo atakosekana golikipa katika timu, mchezaji mmoja wa uwanjani atalazimika kuchukua nafasi hiyo, kwa mujibu wa mwongozo uliochapishwa na Shirikisho la Soka Afrika, CAF.

“Timu ambayo haina wachezaji 11 itazingatiwa kuwa imepoteza mchezo 0-2,” shirikisho hilo lilisema katika taarifa yake hapo jana siku ya Jumamosi. “Katika kesi za kipekee, kamati ya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika itachukua uamuzi ufaao.”

Waandaaji wamesema timu zitaweza kubadilisha wachezaji watano (5) kwa kila mchezo na kubadilisha mchezaji mmoja wa ziada ikiwa mchezo utachukua muda wa ziada.

Timu kadhaa zinazojiandaa kwa ajili ya AFCON zimeripoti kesi za maambukizi ya COVID-19, hususan baadhi ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo, kama vile Algeria, Côte d’Ivoire na Morocco.

Tayari mwenyeji Cameroon amefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2 -1 dhidi ya Burkina Faso kwenye mchezo wa awali uliyomalizika hivi punde.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents