Technology

Fahamu tofauti ya TECNO CAMON 20Premier na INFINIX NOTE 30Vip

TECNO na Infinix ni kampuni zinazofanya vizuri sokoni kwa mwaka 2023, ni kampuni zinaendelea kupambana kujiweka kwenye level nzuri za kuwaburudisha watumiaji wake leo nakuleta comparison Kati ya Infinix Note 30Vip pamoja na TECNO Camon 20premier je simu gani Kali ? 

1) Storage 

Infinix note 30 vip imekuja Ikiwa na storage yenye ukubwa kuanzia 256Gb pamoja na Ram ya 8Gb yenye kuhifadhi vitu ndani wakati TECNO Camon 20Premier imekuja Ikiwa na storage ya 512Gb na Ram 8Gb kwenye kuhifadhi vitu mbalimbali ndani yake Kama vile picha, videos, app, games nk.

Kwaiyo kwenye storage Infinix wako nyuma wakati TECNO wanakupa uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu ndani bila kujaa kwa muda mrefu. ila Infinix wanakupa uwezo wa kuongeza ram na kufanya ufurahie ufanisi kwenye kufanya kazi mbalimbali labda unacheza game, kuperuzi nk.

pia kwenye TECNO Camon 20Premier haijaja na support ya kuweka memory card wakati Infinix Note 30 Vip imekuja na uwezo wa kuweka memory card mpaka kufikia 1Tb kwenye kuhifadhi vitu ndani ya memory card.

2)  Camera 

Kwenye TECNO Camon 20 Premier kamera yake wanakupa mega pixel 50mp +108mp +2mp Ikiwa na sensor ya shift iOS kwa nyuma na mbele ni Megapixels 32mp  wakati Infinix Note 30vip wanakupa 108 +2+ Ai Ikiwa na Akili bandia yenye kukusaidia kuchukua pia kwa ubora kwa nyuma yenye kutoa picha bora Zaidi wakati mbele ni 32mp.

kwenye selfie zote ziko vizuri kwenye kutoa picha Kali wakati Infinix kamera ya nyuma Iko imara Sana kwenye kutoa picha Kali kwenye mazingira yoyote Yale kuliko Tecno. ila Tecno unatumia teknolojia ya shift iOS yenye kutoa picha kwa mfumo wa portrait na kuzuia picha au video kucheza cheza wakati unatumia na kufanya kutoa picha na video kw ubora sana.

3) Battery

Zote zinatumia betri aina ya lipo yenye 5000mah kila moja lakini utofauti wao uko kwenye mfumo wa fast charging ambapo Infinix Note 30 Vip inatumia 68W yenye kuchaji simu na kujaa ndani ya dakika 38 tu toka 1% mpaka 💯 wakati Tecno Camon inatumia 45W Ikiwa na uwezo wa kuchaji chaji ndani ya Lisa limoja na dakika mbili ndo kuja toka Asilimia 1% mpaka 💯.

Pia Infinix Note 30 Vip imekuja na teknolojia ya wireless charging yenye 50W unaweza kushare chaji na rafiki yako kwa kugusanisha tu na kujaa wakati Tecno haijaja na huu mfumo wa wireless reverse charging ndani ya dakika 48 tu simu inaja full.

4) Display 

Zote zimekuja zikiwa na kioo aina ya AMOLED display yenye 120Hz uwezo wa kutizama kitu kwa ubora pamoja Kasi kwenye kufungua kitu kwa haraka, Pia inatumia kiwango kidogo cha umeme kwenye kuonyesha taswira ya kitu, unaona vitu kwa ubora uliomkubwa pamoja na kutunza macho yako kwenye Masuala ya jua na mionzi iliyopo kwenye simu.

kwenye Tecno Camon 20 Premier teknolojia ya fingerprint Iko kwa ndani ya kioo unaweza tumia kutoa lock kupitia kwenye kioo cha simu wakati Infinix Note 30 Vip wao wanakupa fingerprint kwenye button ya kuzima na kuwasha simu pembeni ya simu yako kuweza kutoa lock kwenye kioo chako.

5) Performance

Kwenye mfumo wa processor wote wanatumia processor aina ya mediaTek dimensity 8050 zote ni bora kwenye kucheza game, kuperuzi mtandaoni, kutunza maisha ya betri ivyo ni unaweza kufurahia simu yako kutumia bila kupata moto sana.

pia zote zimekuja Ikiwa na mfumo wa android version 13 kila moja wapo kati ya Infinix Note 30Vip pamoja na TECNO camon 20Premier pia zote Zina support update ya android version 14 unaweza kupakua beta au kusubiria mwezi wa Tisa kupata Original version kabisa.

6) Speaker

kwenye Infinix Note 30 Vip imekuja na speaker za Jbl wakati unasikiliza kitu au kuona kitu unaweza sema uko studio ya millardayo kwenye amplifaya wakati Tecno Camon 20 Premier speaker zake ni za kawaida tu.

zote zinatumia teknolojia ya 5G kwenye kuperuzi vitu mtandaoni kwaiyo mtakua na uwezo wa kuperuzi vitu kwenye Facebook, Instagram, YouTube kwa Kasi kubwa Tatizo la kuganda ganda utaweza kukutana nalo kabisa..

7) Magic skin

TECNO Camon 20 Premier imekuja na teknolojia ya Magic skin kwenye design material yake  yenye uwezo wa kutumika kwenye mazingira yoyote Yani  bila shida yoyote cover lake limeundwa kwa mfumo wa muundo wenye kukusaidia kuweza kulinda kwenye simu yako kwenye mazingira ya vumbi, mafuta nk wakati Infinix haijaja na huu mfumo wa magic skin kwenye Infinix Note 30 Vip. 

unafikiri ni simu gani Kali kuliko mwenzake Kati ya Infinix Note 30Vip na TECNO camon 20Premier tuachie maoni yako ?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents