Technology

Fahamu uwezo uliopo kwenye Kamera ya Infinix ZERO X PRO

Kampuni ya simu Infinix hivi karibuni ilizindua rasmi simu mpya ya toleo la ZERO-Infinix zero x pro. Infinix zero x pro ni simu ya kwanza kwa kampuni ya simu Infinix kuja na camera ya MP108 OIS, zooming lens 60X na AMOLED Screen 6.67 FHD+.
Kupitia Makala hii tutaenda kudadavua kiundani zaidi sifa hizi mpya kwa simu ya kwanza ya Infinix;

KAMERA


Infinix zero x pro imekuja na kamera tatu kwa nyuma, Kamera kuu ikiwa MP108 na kamera nyengine mbili zikiwa na megapixel 8 kila moja. Kamera hizi zinafanya kazi kwa pamoja wakati wa uchukuaji picha, MP108 IOS kazi yake kuu ni kuifanya picha husika kuonekana vizuri kwa kuondoa mawimbi na ukungu wakati wa upigaji picha na hizi kamera nyengine mbili kila moja inakazi yake moja ikisimama kama ulta wide camera na nyengine ni kwajili ya zooming ambayo ina 60x lens.

Faida kuu za kamera hizi kwa pamoja zinampa mtumiaji picha halisi ya kitu, Mtu n.k kutokana na namna ya ufanyaji kazi wa kamera hizi tatu za Infinix zero x pro. Infinix zero x pro inauwezo kwa kurecord video kwa kutumia teknolojia ya 4K lakini pia inauwezo wa kupiga picha ya mwezi kwa kutumia setting za moonshoot camera.

Katika kukamilisha ubora wa picha, Infinix zero x pro imekuja na Quard LED flash, HDR pamoja na panorama.

KIOO
Tukiangalia upande wa kioo Infinix zero x pro imetengenezwa kwa AMOLED SCREEN yenye ukubwa wa inch 6.67 na yenye pixel 1080×2400 ambayo ndio resolution kubwa zaidi inayotumika na simu za bei ya gharamu kama iPhone. Kioo hiki pia kinakuja na refresh rate ya 120Hz na mwanga units 700.

Tembelea https://www.infinixmobility.com/smartphone/zero-x-pro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents