Burudani

Faida ya EP ya Ali Kiba ni hii, wasanii aliowashirikisha ni tishio(Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia EP ijayo ya Alikiba Starter itakayotoka Sept 20.

Anasema kuachia EP amewaza kibiashara kwani itaenda kufungua milango mingine endapo atawekeza kwenye Promo zaidi.

Anasema EP hiyo imeshirikisha wasanii watatu tu au imeundwa na wasanii wanne tu ambao ni Alikiba mwenyewe, Nandy, Jay Melody na Marioo.

Licha ya kuwa Alikiba tayari ameshafanya kazi kadhaa na Marioo pamoja na Nandy wengi wanasubiria kumsikia Alikiba akiwa na Jay Melody.

Tunasubiri kuona pia Alikiba anakuja na ladha/Sound mpya ya muziki au sound ile ile, pia wengi wanasubiria kuona kama EP ya Alikiba itakuwa ya Kimataifa na itaendelea kumuweka Alikiba kwenye sehemu nzuri ya Kibiashara.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents