Fahamu

Familia iliyopoteza watoto tisa kwa siku moja kisa mafuriko

Maziko ya umma yanaendelea nchini Afrika Kusini kufuatia janga baya zaidi la mafuriko kuwahi kutokea nchini humo. Eneo la KwaZulu-Natal ndilo lililoathirika zaidi na mafuriko hayo ni makubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.

Watu 435, wamefariki katika mafuriko hayo ya kihistoria ya mwezi uliopita.Karibu kila kona kuna maombolezo na maziko huku fanyika maziko, ingawa familia nyingine zimeshindwa kuzika ndugu zao kutoka na miili yao kusomba na maji na haijulikani ilipo.

Nje kidogo ya Pietermaritzburg, mamia ya watu wamekusanyika mbele kukiwa na majeneza sita, ukimya ukitawala na nyimbo za maombolezo zikisikika zaidi. Ni nyumbani kwa familia ya Mdlalose. Slindile Mdalose, 43, na Watoto tisa wenye umri wa kati ya miaka 2 mpaka 10 wameuawa katika mafuriko hayo.

Walikuwa wamelala kabla ya mafuriko kuwakuta usingizi na kuwasomba, miili mingine haijapatikana, ikiwa ni zaidi ya wiki mbili tangu tukio hilo kutokea.”Kusema ukweli tumechanganyikiwa, tumekufa ganzi. Hatuwezi kutumia vichwa vyetu. Hili ni jambo kubwa sana kuweza kulielewa,” mjomba wa watoto hao, Thokozani Mdlalose aliambia BBC.

Akiwa amevaa miwani ya giza ili kuficha maumivu yake lakini sauti yake iliyojaa uchungu na mdomo wake unaotetemeka vinasaliti jitihada zake za kuonekana kwamba yhuko sawa na mtulivu.

“Unapolazimika kugawanya huzuni yako, unamfikiria huyu, unamfikiria yule [mmoja]. Ni nyingi sana. Ni vigumu kupoteza mtu mmoja. Ni mbaya zaidi kupoteza wawili. Kumi ni kitu kingine,” anasema.

Funeral
Ndugu na jamaa, wamekuwa wakiomboleza vifo vya watu 435 vilivyotokana na mafuriko KwaZulu-Natal

Mazishi ya misa ya Slindile Mdalose na watoto wake watano – Uyanda, Lubanzi, Ziyanda, Asanele, Lulama – yalifanyika asubuhi yenye baridi. Slindile alikuwa pia shangazi wa watoto wengine wanne, ambao bado hawajapatikana.

“Nikijua kwamba hatuipata miili mingine, pengine inaozea mahali fulani huko nje – maneno hayawezi kuelezea kile kilicho ndani yangu hivi sasa. Siwezi hata kufikiria,” Anasema Bw Mdlalose, aliyepoteza mke na watoto hao.

Anaongeza kuwa watoto hao tisa walikuwa wakicheza kwa furaha na walikuwa wakileta faraja na furaha kwa familia nzima.

Shangazi yao, Nonkululeko Mdlalose, anasema mara ya mwisho alipozungumza na dada yake (Slindile) kwa simu saa chache kabla hajafariki pamoja na watoto wake, aligundua dada yake anaogopa.

Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, hakuna kati yao aliyewahi kushuhudia mvua kubwa ya kiwango hicvho hapo awali. Hata hivyo, hawakutarajia kwamba ingesababisha maafa, Nonkululeko Mdlalose anasema.

“Sijawahi kuhisi uchungu wa namna hii. Nilijiona kuwa mtu mwenye nguvu lakini ninatambua kwamba sivyo, kwamba tutahitaji msaada, natambua tutahitaji ushauri nasaha. Hili ni jambo kubwa sana kwa mtu yeyote kulistahimili,” anaongeza.

Hii ni familia moja tu, mafuriko yameua watu 435, na makumi wengine hawajulikani walipo, wakiziacha familia zao zisijue cha kufanya. Mpaka sasa ni miili chini ya 200 iliyozikwa, huku miili mingine 59 ikiwa bado kwneye mochwari.

Daogs

Taasisi ya kutoa huduma ya mazishi ya Icebolethu, ambayo ni moja ya taasisi kubwa za mazishi KwaZulu-Natal, ambapo hadi sasa imezika zaidi ya watu 70 waliofariki kwenye mafuriko hayo.

Mmoja wa watendaji wake, Mthokozisi Bhengu, anasema maiti hazipo katika hali nzuri( zimeharibika vibaya) kwa sababu ya kuzama kwenye maji, hivyo zinatakiwa kuzikwa haraka ili kuepusha hali zao kuwa mbaya zaidi na zaidi.

“Familia zina mila za kitamaduni ambazo wangependa kufuata, kama familia kuzika ndugu zao kwa wakati mmoja, lakini imetulazimu kuwashawishi wale ambao miili ya wapendwa wao bado haijapatikana, tuendelee kuzika wakati zoezi la kutafuta miili mingine ikiendelea ili kuhifadhi utu wao,” anaongeza.

Floods

Serikali ya Afrika Kusini na wafadhili binafsi wametoa msaada wa kugharamia mazishi lakini mchakato wa madai unasemekana kuwa wa ukiritimba na unaopelekwa polepole, na kusababisha ucheleweshaji zaidi wa mazishi.

Mkuu wa Chama cha Mazishi cha Afrika Kusini, Nomfudo Mcoyi, anasema ucheleweshaji huo ungeweza kuepukika lakini unaongeza zaidi simanzi na huzuni kwa familia.

“Tungeweza kuzika kwa urahisi bila miili kuoza,” anasema Mcoyi akirejea maoni yake kwamba Serikali ina[pasw akushirikisha wataalam tanguhatua za mwanzo za majanga, ili kurahisisha mambo.

Rais Cyril Ramaphosa amekiri kwamba fedha zaidi zinahitajika kuliko iliyotengwa awali dola $68m ili kuujenga upya mji wa KwaZulu-Natal ulioathirika vibaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents