FahamuHabari

Familia ya Jamie Foxx yaarifiwa kuwa tayari kupokea taarifa yoyote mbaya kuhusu Foxx

Maneno yamekuwa mengi sana mtandaoni na wasiwasi mwingi kwa mwigizaji Jamie Foxx, ambaye anaendelea kupata matibabu Hospitalini kufuatia matatizo ya kiafya. Hata hivyo, ni machache sana ambayo yameshirikiwa hadharani kuhusu hali ya staa huyo wa miaka 55.

Mnamo Aprili, familia ya Foxx ilifichua kwenye Instagram kwamba mwigizaji huyo “alipata shida ya kiafya” na kukimbizwa Hospitalini na hii ni kutokana na chapisho lililoshirikiwa na binti yake Corinne, ambalo limeondolewa kwenye jukwaa la Instagram tayari, Foxx baadaye alitoa taarifa yake fupi kwenye Instagram kuhusu kinnachoendelea na afya yake.

inaelezwa kuwa ana tatizo la Kiharusi.

Katika chapisho lake la Instagram lililoondolewa sasa, binti yake  Corinne alisema baba yake alikuwa akipata nafuu.

“Kwa bahati nzuri, kutokana na hatua za haraka na uangalifu mkubwa, tayari yuko njiani kupata nafuu,” ilisema taarifa hiyo. “Tunajua jinsi anavyopendwa na tunathamini maombi yako.

 

Mnamo Mei 3, Foxx alizungumza kwa mara ya kwanza kuwashukuru wafuasi wake kwa wasiwasi wao na kutia moyo wiki kadhaa baada ya tangazo la binti yake Corinne.

“Nathamini upendo wenu wote !!!” aliandika katika chapisho lake fupi lililojumuisha emoji ya mikono na moyo “Kujisikia kubarikiwa.”

Chapisho lake lilipata uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa mashabiki na marafiki na makumi ya maelfu ya maoni yaliyoangazia emoji za moyo na jumbe za kutia moyo.

Lakini chapisho hilo pia lilipata shaka. Watumiaji wengine walijaribu kukisia kile anachoweza kuwa anapitia, wakileta uzoefu wao wa matibabu. Na wengine walisema hawakuamini chapisho la maandishi na wengi Walitaka kumuona hata angepost picha ya usoni tu na kumsikia akizungumza kabla ya kukubali kuwa kweli yuko kwenye nafuu na hii yote ni kutokana na upendo wa wengi.

Sasa habari iliyotolewa asubuhi ya leo ni kuwa familia ya Foxx iwe tayari kupokea taarifa zozote mbaya, hii ina maanisha hali ya kiafya ya staa mkubwa wa Hollywood Jamie Foxx huenda inazidi kuwa mbaya.

Familia bado haijatoa taarifa yoyoyte kuhusu afya ya nndugu yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents