HabariMichezo

FIFA yaifungia Biashara United FC kutosajili 

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) imeifungia Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Biashara United ya Mara kusajili wachezaji kwa madirisha mawili.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya Biashara United kushindwa kuheshimu uamuzi wa awali wa FIFA kuifungia kusajili wachezaji hadi itakapo kamilisha malipo ya madai ya mishahara ya aliyekuwa mchezaji wake Timoth Balton Omwenga.

Kutokana na kutoheshimu uamuzi huo, ndipo FIFA ilipowasilisha suala hilo katika Kamati yake ya Nidhamu ambayo Mei 19, 2022 ilitoa adhabu hiyo kupitia kwa Mjumbe wake Carlos Teran wa Venezuela.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazikumbusha Kuheshimu mikataba zinaingia na wachezaji pamoja na makocha  kwani hiyo ni moja ya vigezo vya kupata Leseni ikiwa ni utelekelezaji wa Kanuni za Klabu (Club Licensing Regulations).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents