FIFA yaifungia Chad

Shirikisho la soka duniani, Fifa limeifungia Chad baada ya serikali ya nchi hiyo kuingilie kati namna ambavyo shirikisho la soka nchini humo linavyofanya kazi.

Hatua hii imekuja baada ya Waziri wa vijana na michezo kuvunja shirikisho la soka nchini Chad mnamo mwezi Machi.

Baada ya tangazo hilo lililotolewa na serikali ya Chad, shirikisho la soka barani Afrika CAF, liliitoa timu ya taifa katika raundi ya pili ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika.

Chad haipo kwenye michuano yeyote ya kimataifa baada ya kuondolewa katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2022 na Sudan mwaka 2019.

Marufuku hiyo itafutwa mara tu baada ya serikali kurudisha uongozi uliyopo na shirikisho hilo kuwa chini ya mamla yake yenyewe.

Related Articles

Back to top button