Figisu zasababisha vijana waliokuwa wakijitolea Iringa kukosa ajira: Ridhiwani

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kuna figisu zimefanyika ili vijana waliokuwa wakijitolea kwa muda wa miaka miwili katika manispaa ya Iringa wasipate ajira.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo jijini Dodoma na Naibu Waziri huyo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum mkoani Iringa, Ritha Kabati.
Vijana hao ambao muda mrefu wamekuwa wakijitolea kufanya kazi za utendaji kwenye mitaa, lakini baada ya ajira mpya kutangazwa waliomba na kukosa kwa madai ya kukosa sifa.
Kikwete amesema kwa mujibu wa taarifa walizopewa vijana hao walionekana wamefeli katika mitihani lakini ukweli ni kwamba kulionekana kuna figisu zimefanyika katika kuhakikisha wamefikia hayo matokeo.
“Ndipo serikali ilipoelekeza kuwa mchakato huo uangaliwe tena upya , ndio maana ninapozungumza hapa hakuna majibu ya wale ambao wamekwishaajiriwa kwa sababu zipo taratibu zinafanyika, Amesema Naibu Waziri Kikwete
Katika swali lake Kabati alitaka kufahamu hatua ambazo zinazochukuliwa kwa baadhi ya viongozi wasiotekeleza matamko yanayotolewa na viongozi wa ngazi ya juu wakiwemo mawaziri.